Je unafahamu nini juu ya uvimbe katika mfuko wa uzazi(Fibroid)?

Uvimbe kwenye mfuko wa kizazi (fibroids ) ni aina ya uvimbe ambao unatokea kwenye mfuko wa uzazi wa mwanawake[uterus].Uvimbe huu unaweza kutokea kwa mwanamke yoyote hasa kwa walio katika umri wa kupata watoto ijapokuwa unaweza kuonekana hata kwa wale ambao wanamiaka  50 na kuendelea.
Uvimbe huu si saratani na hauna tabia ya kubadilika kuwa saratani.Hata hivyo unakuwa katika viwango na ukubwa mbali mbali, kuna watu wanaweza kuwa na fibroid lakini saizi yake ni ndogo hali inayopelekea wasiugundue au wengine wanaweza kuwa na uvimbe mkubwa kiasi kwamba unaweza kumpelekea aonekane kama ni mjamzito.

JE NI MAZINGIRA  GANI AU VITU GANI VINAWEZA KUPELEKEA UVIMBE HUU?

Vitu au mazingira ambayo yanapelekea uvimbe huu bado havijulikani lakini tafiti nyingi zinaonyesha kuwa,vitu vifuatavyo vinawezapelekea mtu kupata fibroids;

  • Historia katika familia.Hii inaelezea zaidi kuhusu kurithi [genetics]
  • 2.Homoni;kuna usibitisho kwamba kiwango kikubwa cha homoni za estrogeni na progesterone zina ushawishi mkubwa katika kukua kwa seli za mfuko wa kizazi hivyo kupelekea fibroids
  • Asili. Tafiti zinaonyesha kwamba wanawake wenye asili ya afrika wako na hatari ya kupata fibroids ukilinganisha na asili zingine
  • Mazingira kama vile kuwa kuvunja ungo pia yanaweza kupelekea mtu kupata fibroid.

Ni vizuri kwenda hospitali  mapema kama utahisi una dalili za fibroids kama zilivyoelezwa katika chapisho linalofuata.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center