Karibu uulize swali na tukuelimishe

Je unaswali lolote ungependa kuuliza kuhusu mada ya Afya Ya Mtoto? Ingia sasa katika sehemu ya comment na uulize swali lako, kwani leo siku ya Jumamaosi kwanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tisa mchana daktari wetu atakuwepo kujibu maswali na kukuelimisha zaidi. Ili kwa pamoja tujenge jamii imara kiafya.

7 thoughts on “Karibu uulize swali na tukuelimishe

  1. Asante kwa Swali lako.

   Kuota meno kwa mtoto inafuata hatua (stages) nne.

   Hatua ya kwanza huanza mtoto akiwepo kwenye mfuko wa kizazi kuanzia wiki sita za umri. Hii ni wakati dutu ya msingi ya jino huundwa.

   Baada ya hapo, tishu ngumu zinazozunguka meno hutengenezwa, karibu miezi mitatu hadi minne ya ujauzito.

   Baada ya mtoto kuzaliwa, hatua inayofuata hutokea wakati jino linatokea nje ya gamu (gum) na kuonekana. Hii Ndio inatokea karibu umri wa mwaka mmoja hadi miaka miwili.

   Hatimaye, kuna upotevu wa meno ya msingi ya “mtoto” na meno ya mtu mzima (permanent teeth) zinaundwa Akifikia umri wa miaka 6 hadi 12.

  1. Kutapika ni sababu ya kawaida kwa watoto kuletwa kwenye chumba cha dharura au kumona daktari. Kutapika inaweza kuwa tukeo la mwili kujikinga na kuondoa vitu vyenye madhara kama toxins, sumu au vimelea. Kutapika kwa muda mrefu au kuendelea kutapika sana inaweza ikawa ni hatari na huweza kutokea na sababu inachohitaji matibabu msingi.

   Kutapika mara kwa mara baada ya kula inaweza kutokea kwa sababu nyingi kwa watoto, ikiwa ni pamoja na chakula kisicho stahili kwa watoto wachanga, athari ya chakula na matatizo ya miundo au kuvimba katika mfumo wa utumbo.

   Kwa watoto wadogo, misuli yanayo sababisha chakula kubaki tumboni (sphincter) ni laini zaidi na husababisha chakula kurudi juu kirahisi, haswa mtoto akila sana au akimeza na hewa mwingi. Inafanana na tukio la ‘reflux’ kwa watu wazima.

   Kutapika inaweza kutokea utumbo au mfumo wa tumbo ikiwa imezibwa na njia ya kawaida ya kupita imekuwa nyembamba. Pia, inaweza kutokea kwa allergy kwa vyakula fulani haswa maziwa ya ngombe, soya, samaki au nyama. Pia, kutapika inatokea ikiwepo infection yeyote ya utumbo (colitis). Haya ni sababu kazaa ya kutapika kwa mtoto; lakini kuna sababu nyingi zingine zinazoweza kusababisha hiyo kutokea.

   Cha muhimu ni kwamba kutapika kawaida inatokea mara moja moja tu au huisha mapema. Ikiwa mtoto anatapika kila akila, mwone daktari wako ili atambue sababu. Wasiliana na daktari wako mara moja ikiwa una mtoto mwenye dalili za kutokomeza maji mwilini, kama kinywa kavu, hakuna machozi au hachezi chezi kama kawaida. Pia fuatilia matibabu ya haraka ikiwa mtoto wako anahisi maumivu makali ya tumbo, ana homa kali, anatapika damu au anachotapika inaharufu ya choo.

 1. Sina swali ila nina advise kuhusiana na Fibroids ,mm sio daktari ila kuna food supplement ambayo inasidia kutokomeza fibroid bila kufanya upasuaji inaitwa C24/7 na Complete Phyto Energizer,dozi ya moja kati ya hizi mbili humaliza kabisaa tatizo la fibroids

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show