“Kisukari kilinibadilisha”

Ilikuwa Aprili 25, 2000, siku mbili zilipita nilikuwa nimeadhimisha kuzaliwa kwangu nikiwa na miaka kumi na tano. Nilikuwa nikisoma katika shule ya sekondari na nilikuwa mwanariadha pia.

“Ikiwa sikuangalia sukari yangu katika damu mara 8 kwa siku, kwa kujichoma kidole changu na kuweka damu kwenye mita ya glucose, niliona nitakufa.”

Nakumbuka dalili zangu za kwanza za ugonjwa wa kisukari. Nilikuwa na kiu wakati wote. Nilihisi kama nilikuwa jangwani na sikunywa maji kwa miaka. Nilikula kitu chochote nilichoweza kupata mikononi mwangu. Kisha nikaanza kujisaidia haja ndogo mara kwa mara, kama mara 20 kwa siku. Nilimwambia rafiki yangu wa karibu kuna kitu kibaya nakihisi lakini sikuwa na uhakika ni nini. Wakati huu mimi pia nilikuwa mchovu, ingawa ilionekana kuwa haijulikani sababu yake. Dalili yangu ya mwisho ilikuwa kupoteza uzito. Mara ya kwanza, nilipoteza uzito kidogo lakini sasa napoteza mwingi.

Wakati nilipogunduliwa na kisukari, muda mfupi baada ya kuanza kupata dalili nilipungua karibia kilo 20. Nilikuwa nimedhohofika sana. Nilikuwa mgonjwa sana. Kwa kipimo cha glucose cha kufunga, kilitambua ndani ya siku inayofuata kwamba nina aina ya kwanza ya kisukari. Yote niliyoyajua wakati huo ni kwamba baadhi ya watu wa kisukari walipaswa kuchomwa sindano na mimi sikupenda kuwa miongoni mwao. Nilikuwa na wakati mgumu kuelewa madaktari.

Ni nini walichokuwa wanasema?

Iliniibidi kuchukua sindano sasa?

Nilielezewa kuwa nilikuwa mtegemezi wa sindano za insulini. Nilishtuka sana. Mshtuko huo utaishi katika maisha yangu siku zote.

Kisukari ni jambo gumu. Kuna watu wengi, labda ambao hawajui ugonjwa wa kisukari na kwamba kuna aina tofauti za ugonjwa wa kisukari. Nawashauri mfike hospitali mapema ukiona dalili zozote za ugonjwa huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center