Kisukari na matatizo ya moyo (PART 2)

Ikiwa nina kisukari nifanyaje kujiepusha na matatizo ya moyo?

Inaelezwa kuwa sababu kubwa ya magongwa ya moyo kwa mgonjwa mwenye kisukari ni kiwango kikubwa cha sukari katika mzunguko wa damu. Hivyo ni muhimu kuzuia ongezeko hili kwa njia mbalimbali ili kujiepusha na uhatarishi wa kupata magonjwa haya, zifuatazo ni njia mbali mbali zinazoweza kupunguza uhatarishi wa kupata magonjwa ya moyo.

1. kufanya mazoezi au kazi ya kukutoa jasho walau kwa dakika 30 kila siku.
2. kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kujua kiwango chako cha kisukari na kupata ushauli sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya
3. kula mlo kamili (epuka vyakula vyenye wanga nyingi na vyenye mafuta mengi)
4. tumia dawa za kisukari kama ulivyoshauriwa na daktari wako (usiache kutumia dawa bila ushauri wa daktari)
5. epuka au punguza matumizi ya pombe, sigara, na madawa ya kulevya
6. tengeneza tabia ya kula matunda yasiyo na sukari nyingi kama matango, matikiti maji na mengineyo.
7. pata ushauri wa daktari haraka iwezekanvyo mara unapo jihisi hali tofauti na kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center