madhara ya kung’oa meno..

Uvumi wa kwamba ‘’dawa ya jino ni kung’oa’’umesababisha meno mengi sana yameng’olewa hata yale ambayo yangeweza kutibiwa na kubaki mdomoni.Watu wengi hufika kwa daktari wa meno kwa lengo moja tu nalo ni kung’oa meno..

Wengi hawafahamu madhara ya kung’oa jino. Kama ilivyo sehemu nyingine ya mwili jino linapoondolewa kuna madhara yanayoweza kumpata mgonjwa hapo baadaye,hivo  huwa inashauriwa kung’oa jino kuwe ni suluhisho la mwisho kabisa endapo matibabu mengine hayawezekani kabisa,haya hapa ni madhara ya kung’oa meno.

 • Kuharibu mwonekano wa mtu hasa meno ya mbele ambapo wengine hukosa uhuru wa kucheka kwa sababu ya mapengo.
 • Kushindwa kutafuna chakula
 • Kuathiri utamkwaji wa baadhi ya maneno kwa mfano maneno yenye herufi S,V na F huwa ni changamoto kutamkwa na mtu aliyeng’oa meno ya mbele.
 • Kurefuka sana kwa jino lilokuwa linakutana na lile lililotolewa mfano uking’oa la chini la juu yake hurefuka sana kuliko kawaida.
 • Mfupa wa taya uliokuwa umeshikilia jino kulika na kusababisha taya kuwa na nafasi kubwa na kusababisha meno mengine yasogee.
meno ya pembeni kupinda,na jino lililobakia kurefuka zaidi.
 • Kusababisha ngozi na misuli ya uso kulegea mapema na mtu kuonekana mzee kuliko umri wake.
 • Kusababisha matatizo kwenye maungio ya taya la chini na mifupa ya kichwa yaani(temporalmandibular joint dysfunction) jointi hii inapatikana usawa wa tundu la sikio unaweza kuhisi inavofanya kazi kwa kuweka mkono maeneo hayo na kufungua mdomo.
jaribu kujishika maeneo haya pande zote mbili na fungua mdomo kuihisi jointi hii

Inashauriwa  kufanyiwa uchunguzi wa kinywa na meno angalau mara mbili kwa mwaka hii itasaidia kugundua matatizo ya meno  mapema ya kuyatibu kabla jino halijafika hatua ambayo suluhisho pekee ni kuling’oa.Kama tayari ulikwishang’oa jino usihofu,unaweza kuweka meno bandia ambayo yatakusaidia kutafuna na kufanya kazi zingine kama meno asilia na kuepuka baadhi ya madhara,endelea kufuatilia mada zetu hivi karibuni tutazungumzia kwa undani kuhusu meno bandia.

15 thoughts on “madhara ya kung’oa meno..

 1. Ahsante sana flaviana nimejifunza kitu kipya kuhusu afya ya meno
  Swali: je kunamadhara gani kwa MTU anayenga’risha meno

  1. Karibu sana Fanuel,madhara ya kung’arisha meno yanategemeana na njia gani inayotumika kuyang’arisha tutazungumzia kwa undani njia hizo hapahapa usikose kusoma,lakini changamoto kubwa huwa ni meno kupungua uimara wake.Madhara mengine ni madogomadogo na huwa si rahisi kutokea moja kwa moja lakini faida za kung’arisha meno ni nyingi zaidi hivyo huwa tunashauri kama unaona meno yako hayakuridhishi fanya matibabu mpka utakapoona inafaa.

 2. Asante sana daktari topic nzuri sana hii napenda kujua ni baada ya mda gani ndo nashauriwa kuvaa meno bandia nikishatoa jino langu

  1. Asante fortunata kwa swali zuri,kulingana na aina ya meno bandia ambayo muhusika anatumia huwa tunaweza kusema mtu asubiri kwa muda gani,lakini kwa watanzania wengi wanatumia meno bandia ya kutoa na kuweka yani (removable denture) hizi zinaweza kuanza kutumika baada tu ya pengo kupona,lakini yafaa kushauriana na daktari wako kabla hujang’oa jino njia nzuri ya kupata meno bandia,ijengeke tabia kuwa mtu aking’oa jino awe ameshapanga kuweka jingine ili kuepuka madhara tajwa.

 3. nashukuru nazani ni elimu nzuri sana kwa wagonjwa pia kwa watu wote kwani weng tumekuwa tukielewa tu kwamba uking’oa jino madhara ni kubaki pengo tu but leo nimetambua madhara mengine ambayo ni hatari zaid. keep it up. and be blessed

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show