“Mimi ninangozi nyeusi, siwezi kupata saratani ya ngozi”

Hii ni kauli ambayo inaaminika na watu wengi. Lakini kihalisia iko mbali sana na ukweli. Saratani ya ngozi ni ugonjwa ambao anaweza kuugua mtu yoyote hata yule mwenye ngozi nyeusi. Ngozi nyeusi inakiasi kikubwa zaidi cha melanini, hali ambayo inafanya watu wenye ngozi hizo kupata ulinzi zaidi dhidi ya mionzi ya jua kuliko watu weupe. Lakini hii haimaanishi kuwa mionzi hii ya jua haiwaathiri watu weusi. Ki uhailisia watu weusi pia wako katika hatari ya kupata saratani ya ngozi hasa kutokana na imani kuwa haina haja kujikinga na jua na pia kutokana na dalili za ugonjwa kujificha zaidi kwa watu weusi. Kukaa juani kwa muda mrefu hasa kati ya saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni huongeza hatari ya kupata saratani ya ngozi. Hivyo inashauriwa kukaa ndani au katika sehemu yenye kimvuli mida hiyo. Kama unashughuli ambayo inakubidi kukaa juani inashauriwa kuvaa mavazi yanayofunika ngozi, kofia pamoja na miwani ya jua ili kujikinga na mionzi ya jua ya moja kwa moja. Vile vile inashauriwa kutumia losheni za jua kadiri ya maelekezo kila ambapo unaenda juani. Saratani ya ngozi ni ugonjwa hatari na ni muhimu sana kujilinda dhidi ya ugonjwa huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center