Nifanyaje endapo nina uvimbe kwenye kizazi?

 

  • Ili kujua kama una uvimbe kwenye kizazi, daktari wako ataangalia kizazi kwa kutumia kipimo cha ultrasonographia ili kuuona uvimbe
  • Pia ataangalia wingi wa damu, kwani uvimbe mara nyingine hupelekea kutokwa kwa damu nyingi sana hasa wakati wa siku zako za mwezi (hedhi) .
  • Tiba juu ya uvimbe kwenye kizazi hasa kama bado unapenda kupata watoto, ni kufanya upasuaji wa kutoa uvimbe.
  • Mda mwingine uvimbe huwa mkubwa sana,kiasi kwamba inabidi upasuaji kufanyika kutoa uvimbe pamoja na mfuko wa uzazi.
  • Pia Kuna tiba ya vidonge ambavyo hutumiwa kupunguza ukubwa wa uvimbe. Japokuwa tiba hii hutolewa hasa kama uvimbe bado ni mdogo.
  • Asilimia ya wanawake wanaokumbwa na tatizo hili la uvimbe kwenye kizazi inaongezeka kwa kasi hasa kutokana na mtindo wa maisha tuliyonayo sasa.
  • Jambo la muhimu kuliko yote ni kujitahidi kwa nguvu zote kuepuka hasa athari zinazotokana na uvimbe huu.
  • ugunduzi wa uvimbe mapema ndio jambo la muhimu hasa kuokoa kizazi chako.
  • Jijengee tabia ya kumtembelea daktari wako mara kwa mara kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Privacy Preference Center