Je, nikiwa na kisukari naweza pata magonjwa ya moyo? (PART 1)

Mgonjwa wa kisukari mbali na kua katika hatari ya kupata magonjwa ya macho, figo na mengineyo, huwa katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo.
Hali inaelezwa kusababishwa na ongezeko kubwa la sukari mwilini hivyo kuharibu mishipa ya damu, inayosambaza damu kwenye misuli ya moyo. Hivyo misuli ya moyo kukosa hewa safi ya oxygen na chakula cha seli, hali hii husababisha misuli ya moyo kushindwa kusukuma damu vizuri katika mwili.

Hali hii inaelezwa kuhusishwa sana na wagonjwa yenye hali zifuatazo
1. kuwa na uzito mkubwa
2. kutofanya mazoezi au kazi yoyote ya kukutoa jasho
3. kua na kiwango kikubwa cha mafuta aina ya cholesterol mwilini
4. kuacha kutumia dawa za kisukari kwa muda mrefu bila kushauriwa na daktari
5. kutumia vyakula vya mafuta na wanga nyingi
6. kuvuta sigara na kutumia pombe kupita kiasi

Mara upatapo dalili zifuatazo ni muhimu kumuona daktari kwa ajiri ya vipimo na ushauli zaidi
1. kupumua kwa shida hata bila kufanya kazi au mazoezi
2. kuchoka kwa urahisi
3. kikohiozi wakati wakulala chali
4. maumivu ya kifua hasa upande wa kushoto
5. mapigo ya moyo kwenda mbio
6. kizunguzungu na kichwa kuuma

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center