Ningependa kupona Kisukari kabisa (Part 1)

Rafiki yangu aliongea na mimi siku moja kwa masikitiko makubwa sana na kusema kwamba baba yake ana kisukari na angetamani nimsaidie kumpatia tiba ili apone kabisa. Hili ni tamanio la wengi kwa kuwa huwa tunaambiwa kuwa kisukari ni ugonjwa endelevu na huambatana na matatizo ya moyo, figo, macho, mishipa ya fahamu na haya yote hupelekea hali kuwa mbaya zaidi mwisho wa siku.

Wengi huuliza maswali kama;

  • Je kisukari hutibika kabisa!?
  • Je naweza kutibu kisukari!? Kama ndiyo je ni kwa njia gani!?
  • Wengine wanasema kisukari kinatibika ila daktari ameniambia hakuna tiba. Je kipi ni sahihi!?
  • Je nafanyaje kutibu kisukari!? Wengine wanasema hakuna tiba ila mimi siwaamini.
  • Je inawezekana kutibu kisukari kwa kubadilisha chakula na aina ya maisha!?
  • Kwani kisukari hakiwezi kutibiwa kwa kutumia dawa za mitishamba!? Na je naweza kuacha dawa na kujaribu kitu kingine!?

Baada ya kuangalia maswali hayo machache wengi mtatamani nitoe jibu la mwisho na niachane na simulizi nyingi. Jibu ni kwamba kisukari hakitibiki. Mara ugundulikapo na ugonjwa wa kisukari basi wewe utakua na ugonjwa huo siku zote.

Hata hivo tafiti zinaonesha kwamba mtu mwenye kisukari anaweza kupata rehema (remission) au mabadiliko (reversal) na kudhani kwamba amepona kabisa. Hii hutokea pale ambapo mtu anaweza kudumisha kiwango cha sukari kwenye damu kama mtu asiye na kisukari huku akiwa ameacha kutumia dawa zote au baadhi, matokeo haya anakua anayapata kwa kupitia chakula na mabadiliko ya aina ya maisha.

Hii ni tofauti na kudhibiti kisukari kwani mtu akisema amedhibiti kisukari anakua anachanganya matumizi ya dawa, chakula na mabadiliko ya maisha.

Itaendeleaโ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆโ€ฆ

Privacy Preference Center