Ningependa kupona Kisukari kabisa (Part 2)

Kubadilisha hali yako ya kisukari siyo jambo linaloweza kutokea ndani ya usiku mmoja. Inahitaji malengo na kujituma na hii itakusaidia kupunguza uwezekano wa matatizo yatokanayo na kisukari. Kudumisha kiwango cha sukari cha kawaida kwenye damu ambacho ni;

  • 4-6 mmol/l ikiwa hujala masaa 8 au zaidi au
  • 7.8 mmol/l au chini ya hapo ikiwa ni muda wowote au masaa mawili baada ya kula.

Njia zipi sasa nitumie!?

 

1. Matumizi ya mlo wenye kiasi kidogo cha wanga
Huu ni ule mpango mzima wa uchaguzi wa chakula kutoka kwenye yale makundi ya vyakula kulingana na upatikanaji na jinsi ya kupima chakula chako kama ilivoelezewa kwenye makala ya  http://daktarimkononi.com/2018/02/11/nile-nini-endapo-nina-kisukari-part-2/

2. Matumizi ya mlo wenye kiasi kidogo cha kalori
Mlo wenye kiasi kidogo cha kalori mara nyingi hutumika ili kumsaidia mtu kupunguza uzito kwa kilo 0.5-0.9 ndani ya wiki moja. Hii huwa inajumuisha kupunguza kiasi cha mafuta kwa zaidi ya 20-35% ya kiasi chote cha kalori unachotumia, kula wanga mchanganyiko kama vile nafaka zisizokobolewa, mbogamboga na matunda, kutumia protini zenye kiwango kidogo cha mafuta kama samaki, kuku, mimea jamii ya kunde (maharage, njegere, njugu), vyakula vyenye kambakamba (fibres).
Ulaji huu unahitaji vipimo maalumu kwa kila aina ya chakula na unahitaji usimamizi wa mtaalamu hasa wa lishe ili kuzuia mtu asipate lishe duni.

3. Upasuaji (Bariatric Surgery)
Hii inahusisha upasuaji unaopunguza kiasi cha chakula kinachoweza kubebwa na tumbo au kuzuia umeng’enywaji mzuri wa chakula na kupelekea kupunguza uzito na kupunguza uwezekano wa kupata athari za kisukari. Hata hivyo hii inatakiwa kuwa njia ya mwisho kuifikiria.

“muhimu unatakiwa kujua kwamba kisukari huwa hakisubiri, usipofanya kitu chenyewe kinaendelea”

Privacy Preference Center