Je nifanye nini endapo kinywa changu kinatoa harufu mbaya kutokana na kisukari?

Kwanza kuna sababu nyingi ambazo husababisha kinywa kutoa harufu mbaya, moja wapo ni kuwa na ugonjwa Wa kisukari. Mtu mwenye tatizo la kinywa kutoa harufu mbaya kutokana na kisukari ni vigumu kwake kutambua kuwa ana tatizo hilo ingawa tatizo hilo linaweza kutibika kirahisi.

Kitu cha kufanya endapo una tatizo la kinywa kuwa na harufu mbaya kutokana na kisukari;
1.Hakikisha kiwango cha sukari kwenye damu ,kipo katika kiwango kinachohitajika. Ambapo inatakiwa kuwa na mlo kamili Wa chakula na kuepuka kula vyakula vyenye sukari vya kutengenezwa. Mwili hauwezi kutengeneza hormoni ya insulini ili kushughulikia sukari iliyoingia mwilini. Hivyo inampasa mtu ale vyakula vyenye sukari asilia ambavyo haviwezi kuathiri afya yake. Ambapo itasaidia kupunguza sukari nyingi mwilini na ivyo kinywa kuto kutoa harufu mbaya hata kama unakisukari.

2.kunywa maji kwa wingi kwa siku, ambapo kiwango cha chini ni nusu gallon kwa siku na epuka kula matunda, Jussi na soda vilivyo na sukari nyingi.

3.Fanya mazoezi Mara tatu kwa wiki. Kufanya mazoezi kutakusaidia uwe mnywaji Wa maji mengi mchana na hivyo kupunguza kutoka kwa harufu mbaya kinywani.

Endapo umefanya yote haya na Hali haijabadirika, kamwone daktari kwa matibabu zaidi .

Privacy Preference Center