Ugonjwa wa Kisukari kwa Watoto

Kisukari kwa watoto(Type 1 diabetes) kinatokana na upungufu wa insulini.

Upungufu huu unatokea pale kinga ya mwili inaposhambulia    celi (aina ya Beta)  kwenye kongosho (pancreas) na kupelekea kushindwa kabisa kutengeneza insulini.

Uwezekano wa kupata ugonjwa huu huongezeka pale panapokuwa na ndugu wa karibu mwenye kisukari.

Dalili hutokana na kuwepo kwa sukari ngingi mwilini ambayo husababisha

  • Kusikia kiu marakwamara
  • Kukojoa sana bila kunywa maji mengi
  • Kusikia njaa mara kwa mara
  • Kupungua uzito na kudhohofika

Tafiti zinaonyesha watoto haswa chini ya miaka 5 wanahatari kubwa ya kuchelewa kugundulika.

Hivyo ni muhimu kuchunguza hasa pale mtoto anapo ugua mara kwa mara na kupata mashambulizi ya fangasi .

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center