Fahamu kuhusu meno bandia.

Meno hufanya kazi mbalimbali  kinywani. Kazi kubwa huwa ni  kutafuna chakula,pia husaidia katika kuongea na kutegemeza  misuli na ngozi inayozunguka  kinywa.Ikitokea meno yakaharibika na kuondolewa kinywani,kazi hizi hushindwa kufanyika kwa usanifu hivo inashauriwa mtu kutumia meno bandia ili kuweza kuzifanya kazi hizo. 

kuna aina 3 za meno bandia nazo ni:

  • Meno ya bandia ya kuvaa na kuvua(removable partial denture)
  • Meno ya kugandisha (fixed dentures)
  • Vipandikizi (implants)

Leo tutaangalia aina ya kwanza ya meno bandia.

meno bandia ya kuvaa na kuvua

Haya  ni yale ambayo mtumiaji anaweza kuvaa,kuvua na kuyasafisha kila siku.Meno haya  ni mbadala wa meno asilia. Yanaweza  kuwa ya mdomo mzima (full denture) ambayo hutumiwa na wasiokuwa na meno kabisa(vibogoyo)  au baadhi ya meno katika kila taya (partial denture).

Faida za meno bandia

  • Kutafuna vyakula mbalimbali visivyo vigumu sana.
  • Kutabasamu na kuongea vizuri.
  • kupendezesha mwonekano wa mtu,kuzuia ngozi na misuli kulegea

 

meno bandia hurejesha tabasamu na kupendezesha mwonekano

Meno ya bandia hutengenezwa kwa kadiri ya uhitaji,uwezo wa kifedha pamoja na hali ya kiafya. Hii ni baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu  na kutibiwa  matatizo mengine kama meno yaliyotoboka na magonjwa ya fizi kisha daktari atachukua vipimo kwa ajili ya kutengeneza meno hayo.Meno ya bandia huweza kutumika katika kipindi cha mda mrefu kulingana na aina au meno husika.Lakini kikubwa zaidi ni kuzingatia masharti ya utunzaji wa meno hayo.

 


Anneti Ronald DDS 5 🇹🇿

"The going is tough , but the tough gets the going"

All author posts

Privacy Preference Center