Je, sababu zinazoweza kupelekea tatizo hili ni zipi? (part 2)

Sababu zinazoweza kupelekea tatizo hili huweza kujitokeza kabla ya kuzaliwa kwa mtoto kama ifuatavyo:

  • Mama mjamzito kutoka na damu kwenye uke kabla ya kujifungua.
  • Presha kuwa juu wakati wa ujauzito.
  • Umri mkubwa wa mama mjamzito zaidi ya miaka 35.
  • Ujauzito wa mapacha.

Pia sababu zinazoweza kupelekea tatizo hili wakati wa kujifungua ni:

  • Mtoto kutanguliza makalio wakati wa kujifungua.
  • Leba inayochukua mda mrefu zaidi ya masaa 18.

Sababu hizi ni hatarishi hasa kwa sababu zinaathiri upatikanaji wa oksijeni kwenye ubongo wa mtoto.

Tiba:
Hakuna tiba mbadala, ila unaweza kuepukika kwa mama mjamzito kuudhuria clinic kwa wakati ili aweze kutatua shida kama presha.
Na mtoto mwenye utindio wa ubongo anapaswa kufanyiwa mzoezi ya viungo pamoja na kupata elimu katika vituo maalumu, kwani hii itamsaidia kuwa na afadhali katika kuongea na kutembea.
Na mwisho kabisa anaweza kupata dawa kwa ajili ya kulegeza misuli iliyokaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center