Mtoto mwenye utindio wa ubongo (part 1)

Utindio wa ubongo ni hitilafu inayotokea katika ukuaji wa ubongo wa mtoto kabla haujakomaa. Itilafu hiyo inaweza kutokea kabla mtoto hajazaliwa, wakati wa kuzaliwa,hata mara baada ya kuzaliwa. Sababu kuu ni ukosefu wa hewa ya oksijeni kwenye ubongo wakati unajitengeneza.

DALILI ZAKE.
Kulingana na sehemu ya ubongo iliyoathiriwa katika ukuaji wake mtoto ataonyesha dalili kama
1.Misuli ya miguu na mikono kukaza sana au kulegea sana kuliko kawaida
2.Mtoto kushindwa kukua kwa wakati unaotegemewa kama ifuatavyo:

  • kushindwa kuongea, kutambaa, kukaa, kutembea ,kucheza na watoto wengine.
  • Na kwa kuwa ubongo umedumaa hushindwa kukua kiakili na hivyo kushindwa kufikiri na kujifunza kitu chochote.

Na dalili hizi huonekana kabla mtoto hajatimiza miezi 18.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center