Fahamu kuhusu Iskemia ya papo hapo kwenye miguu

-Iskemia hutokea endapo damu inayofika katika sehemu ya mwili ni kidogo (au kutokufika) na kusababisha seli kuathirika kwa kukosa oksijeni hivyo kupelekea kufa kabisa. Hali hii hutokea katika sehemu mbalimbali za mwili kama vile mikono,miguu,moyo n.k.

Iskemia inagawanyika katika makundi mawili

 1. Iskemia ya papo hapo(acute)
 2. Iskemia sugu(chronic)

-Iskemia ya papo hapo(acute) ya miguu hutokea kama damu isiyo ya kutosha inapofika katika mguu au damu isipofika kabisa, na hutokea ghafla.

Sababu hatarishi za iskemia ya papo hapo ni kama zile za iskemia sugu nazo ni

 • Mafuta mengi mwilini
 • Kisukari
 • Uvutaji sigara

Lakini ili itokee ghafla husababishwa na sababu zifuatazo

 • Damu iliyoganda inapoziba mishipa ya damu na kuzuia damu kupita
 • Mafuta kwenye kuta za mishipa ya damu
 • Mgandamizo kutoka nje unaokandamiza mishipa ya damu
 • Kukatika kwa mishipa ya damu kwa sababu ya kujeruhiwa, mfano katika ajali

Dalili zinazotokea kwa mtu anayepata tatizo hili ni zifuatazo

 • Maumivu
 • Kuhisi ganzi
 • Kuhisi ubaridi kwenye miguu
 • M(Mi)guu kubadilika rangi na kuwa rangi ya weupe au bluu iliyopauka
 • Pia miguu inaweza kupooza

Mara uonapo dalili ni vyema kutembelea kituo afya ili kupata uchunguzi na kujua nini kimesababisha pia utaweza pata tiba stahiki. Kufika kituo cha afya pia itasaidia kujua kama kuna shida nyingine tofauti na iskemia na kuepuka madhara makubwa yatokanayo na iskemia kama vile miguu kuoza. Matibabu yanaweza kuwa ya kutumia dawa au upasuaji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center