Fahamu sababu za moyo kutanuka na dalili zake

Moyo hutanuka kutokana na kusukuma damu kwa nguvu zaidi kulingana na hali ya kawaida..
Zifuatazo ni sababu zinazopelekea hali hii
1. Kupanda kwa shinikizo la damu. Hii hufanya moyo isukume damu kwa nguvu zaidi ili kuifikisha mahali husika na kusababisha misuli ya moyo kupanuka hasa ventrika ya kushoto
2. Magonjwa ya moyo kama Amyldosis, protein ambazo hukaa ndani ya mishipa ya damu na kufanya moyo usukume damu kwa nguvu zaidi
3. Maji kujaa katikati ya kuta za moyo
4. Unene uliopita kiasi unaosababisha mafuta kuganda ndani ya mishipa ya damu na kuongeza presha ya mwili

Dalili za moyo kupanuka ni kama zifuatazo

  • ย mapigo ya moyo kwenda mbio
  • kupumua harakaharaka
  • kupata shida ya kupumua hasa baada ya kazi nzito au ukilala chali usiku
  • maumivu ya kifua
  • kuchoka bila sababu
  • kuvimba miguu na tumbo au mwili mzima
  • kuongezeka uzito

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center