Kijue kiharusi (stroke) kitokanacho na shinikizo la damu (hypertension)

Presha ya juu (high blood pressure) isipodhibitiwa kwa muda mrefu huweza kuathiri hali ya afya ubongo.
Hii hupelekea mtu kupata kiharusi (stroke) ambapo mtu anaweza pata udhaifu wa miguu na mikono upande mmoja wa mwili hivyo kushindwa kutembea, mdomo kupinda upande mmoja na wakati mwingine kushindwa kuongea.
Pia mtu anaweza pata maumivu makali ya kichwa na kushindwa kuona vizuri. Hizi dalili huambatana na presha ya mwili kuwa juu (high blood pressure).

Ili kuepukana na tatizo hili inashauriwa kwa mgonjwa mwenye shinikizo la damu (hypertension) kujenga mazoea ya kupima presha mara kwa mara na kutumia dawa na masharti kama inavyoshauriwa na madaktari.

Endapo mtu mwenye shinikizo la damu atapata dalili hizo hapo juu, ni vema akafika mapema kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kwa haraka iwezekanavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center