Shinikizo la damu linaweza kuleta upofu

Shinikizo la damu limekuwa ni tatizo katika karne za hivi karibuni, ikiwa ni sababu nyingi zilizopelekea ongezeko hili hasa mfumo wa maisha wa watu wengi. Mbali na athari nyingi kama matatizo ya figo na kusababisha kiharusi,shinikizo la damu laweza pelekea pia matatizo ya macho mpaka upofu kabisa. Hii hutokea hasa pale shinikizo la damu likiwa kwa muda mrefu na halijatibiwa au pale mtu anapoendeleza mfumo mbaya wa maisha unaongeza hatari ya kupata shinikizo la damu.
Athari katika jicho na mfumo mzima wa kuona hutokea pale mirija ya damu ya damu hasa sehemu ya nyuma ya jicho yaani retina inapopata hitilafu. Na kwa kawaida ni katika sehemu ya retina ambapo picha inayotazamwa hutengenezwa .
Nini hutokea mpaka mirija ya damu kuharibika?
Hii hutokea pale kuta za mirija ya damu kwenye retina inapotanuka,hivyo kufanya mirija hiyo kuwa na kipenyo kidogo na kuzuia damu ya kutosha kupita na kufika kwenye retina . Na hii husababisha usambazaji mdogo wa oksijeni katika eneo lile na hata kupelekea retina kuvimba na damu kuvia pale mirija inapopasuka. Zaidi ya hapo ukubwa wa shinikizo la damu na kuvimba kwa retina yaweza kusababisha mgandamizo kwenye mishipa ya fahamu ya jicho na hapa ndipo mtu anaweza kupoteza uwezo wa kuona kabisa.
Dalili huwa ni kama ifuatavyo;
-jicho kuvimba
-kuona mbili mbili[double vision]
-kuona mawingu ,picha isiyo vizuri
-kichwa kuumwa.
Njia kuu ,ya kutibu ni kufuatilia vyema presha yako yaani utumiaji sahihi wa dawa na pia waweza kuzuia kupatwa na tatizo hili kwa kufanya yale yote yatakayosaidia katika kupunguza shinikizo la damu kama mazoezi na ulaji wa vyakula vya afya.

2 thoughts on “Shinikizo la damu linaweza kuleta upofu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center