Kuzimia au Kuzirai

KUZIMIA AU KUZIRAI
Kuzimia/kuzirai ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mfupi ambapo huambatana na kushindwa kusimama kwa muda huo na kupelekea kuanguka japo mtu huweza kupona au kurudi katika hali ya kawaida bila uhitaji wa tiba.

Kuzimia/zirai kunaweza pelekea ulemavu kutokana na kuanguka au ajali zitokanazo na kuzimia/kuzirai.

Kwa nini tuzungumzie kuzimia/zirai?
Kuzimia/zirai ni kati ya vitu ambavyo hutokea kila siku katika maisha ya mwanadamu, inaweza tokea wakati wa msiba, wakati wa kuangalia mpira, kwenye maandamano, na sehemu nyingi zaidi.

Mara ya kwanza kumuona mtu aliyezimia/zirai ilikuwa ni wakati nipo shule ya msingi na kulikuwa na kuhusishwa kwa wanaozimia/kuzirai na   imani potofu kama (wanamajini au kulogwa)

Lakini baada ya kuanza kusomea udaktari imani hiyo imebadilika na hii ni kutokana na kujua vitu vinavyopelekea mtu kuzimia au kuzirai na kuelezwa kwa kina ni kwa nini mtu anazimia au anazirai mara kwa mara na viashiria vipi ambavyo ukiviona inabidi umuwahishe aliyezimia/zirai hospitali au katika kituo cha afya haraka iwezekanavyo.

Je bado unaamini aliyezimia amelogwa au anamajini kama huko mwanzo basi napenda kukuambia ni vyema tukajua vinavyosababisha mtu kuzimia”

-kukosekana au kushuka kwa kiwango cha sukari (glucose)

-kupungua au kusimama kwa mzunguko wa damu katika ubongo

-kushindwa kupumua au ukosefu wa oksijeni kwenye ubongo

-uoga, msongo wa mawazo na  maumivu makali

-kusimama kwa muda mrefu

-Kupungua maji mwilini na

-matumizi ya pombe

-matumizi mabaya ya dawa za kushusha presha

-Kukaa muda mrefu kwenye jua

-Kuona au kugusana na damu.

Huduma ya kwanza kwa mtu aliyezimia au kuzirai.

-mlaze chali aliyezimia au kuzirai chini.

-kunja miguu yake au iinue ili kuongeza mzunguko wa damu kwenye ubongo

-mpunguzie nguo zinazombana ili kurahisisha mzunguko wa damu.

-Jaribu kumuamsha kwa kumuita kwa sauti ya juu.

-Mlaze kwa ubavu kama anatapika au anatokwa na damu mdomoni.

Dalili za mwanzo anazokuwa nazo mtu anayetaka kuzimia/kuzirai.

-kujisikia kizunguzungu
-kushindwa kuona vizuri
-kichefuchefu
-kutokwa Jasho.

Muwahishe aliyezimia au zirai haraka hospitali au katika kituo cha afya kama ni mjamzito au anajulikana kuwa na magonjwa ya moyo”

6 thoughts on “Kuzimia au Kuzirai

  1. Shukrani kwa kuuliza swali.
   Moja kati ya sababu ambazo zinaweza changia mtu kuzimia kwa wanaoombewa ni kusimama kwa muda mrefu pamoja na uoga.
   Pia inategemea na maombi hayo yanafanyika wapi kama ni sehemu yenye jua na wamekaa kwa muda mrefu basi inawezekana mtu akazimia.
   Shukrani na natumai umeweza elewa.
   Kama una swali lingine usisite kuuliza
   Asubuhi njema.

  1. Shukrani kwa kuuliza swali.
   Kuona au kugusa damu inapelekea mtu kuzimia au kuzirai kutokana na ule uoga unaojengeka wakati wa kuona damu hii husababisha kemikali aina ya acetylcholine kutowela na mwili ambayo hufanya mishipa ya damu kutanuka na mapigo ya moyo kuenda taratibu hivyo hupelekea upungufu wa damu kwenye ubongo na hivyo mtu kuzimia.
   Karibu sana daktari mkononi na kama hujaelewa maelezo hayo unaweza uliza na tukajitahidi kujibu.
   Uwe na siku njema.

  1. Habari
   Shukrani kwa swali
   Mtu aliyezimia hakomi kupumua bali anakuwa kapoteza fahamu ila anaendelea kupumua kama kawaida.
   Kujua kama amezimia au la unaweza kujaribu kumuita pamoja na kumgusa kuona kama anajibu.
   Pia unaweza jua mtu kazimia kama uliona anadalili za kutaka kuzimia.
   Shukran na karibu tena daktari mkononi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show