Chakula bora na kupunguza uzito

Kumekua na tabia ya kupunguza uzito kwa kuacha kula milo kamili, mfano badala ya milo mitatu kwa siku anakula mlo mmoja. ย 

Hii njia siyo sahihi, kwa sababu utakua unautaabisha mwili tu. Ambacho unatakiwa kufanya ni hakikisha unakula milo mitatu bila kuruka, ย ila aina ya chakula inabidi ubadili.

Zifuatazo ni aina za chakula ambazo ni sahihi zaidi kama unataka kupunguza uzito.

 

1: Epuka vyakula vyenye mafuta mengi. Vyakula kama nyama zenye mafuta mengi au vyakula vya kukaangwa viepuke. Badala ya kula nyama zenye mafuta kula mimea yenye mafuta kama maparachichi.

2: Punguza ulaji wa nyama nyekundu( wanyama wenye miguu minne kama ng’ombe) ย badala yake kula nyama nyeupe (samaki na kuku).

3: Kula vyakula vya wanga kama ugali na wali lakini epuka vyakula vilivyokobolewa sana kama ugali wa sembe badala yake kula dona

4: Ongeza kula mboga za majani na matunda kwa wingi zaidi.

5: Kunywa maji mengi badala ya kunywa vinywaji vilivyosindikwa kama soda. Kunywa angalau lita 1.5 kwa siku. Usinywe maji ya baridi sana hasa yaliyotoka kwenye jokofu.

6: Hakikisha unapata usingizi wa kutosha sio chini ya masaa sita na pia usizidishe muda wa kulala.

7: Pia jitahidi kufanya mazoezi ya viungo.

Endelea kupata ushauri sahihi juu ya mazoezi kupitia tovuti yetu, pia uliza maswali inapowezekana.