Dawa za uzazi wa mpango za dharura (P-2); part1.

Hizi ni dawa zinazotumika kuzuia mimba za ghafla endapo zikimezwa ndani ya masaa 72 baada ya tendo la ndoa( bila kinga).
Dawa hizi huzuia mimba kwa kuzuia au kuchelewesha kutolewa kwa yai, kuchavushwa kwa yai na kuzuia upandikizwaji wa kijusi katika mfuko wa uzazi.
Dawa hizi haziharibu mimba iliyokwisha tengenezwa hivyo ukichelewa kumeza dawa hizi zinakua hazina msaada.
Dawa hizi huzuia mimba kwa takribani 95% zikimezwa ndani ya masaa 24 baada ya tendo la ndoa na 58% kama zikimezwa baada ya masaa 48 au 72.
Yafuatazo ni baadhi ya madhara ya dawa hizi;
1. Kichefuchefu na kutapika
2. Maumivu ya tumbo
3. Maumivu ya kichwa na kizunguzungu
4. Kutoka damu ukeni
5. Mabadiliko katika mzunguko wa hedhi endapo mtu anatumia mara kwa mara.
Hivyo ni muhimu kutumia hizi dawa pale tu inapobidi kisha kutafuta njia za uzazi wa mpango za kudumu na zilizo nafuu kwa afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center