Huduma ya kwanza kwa mtu anayetokwa na damu

Ajali ni tukio  ambalo hutokea ghafla, kwani inaweza kumpata mtu yeyote na wakati wowote bila kujianda. Inaweza ikawa ofisini, nyumbani, shambani, shuleni na barabarani. Asilimia kubwa ya watu hawajui jinsi ya kutoa huduma ya kwanza, kwa mfano tunaona wenzetu wengi wanakufa kwa sababu ya kukosa msaada pale inapotokea ajali aidha ya gari, pikipiki, kujikata na kitu chenye ncha kali na kadhalika.

Mtu aliyepata ajali huweza kumsababishia kupata majeraha na kuvuja damu kidogo au nyingi, kama ajali hii itatokea mgonjwa atatakiwa kuhudumiwa mapema sana kwani kama akicheleweshwa anaweza akafa. Na mtu huyu huweza kuwa na dalili zifuatazo:

 • Kupumua kwa shida
 • Kupatwa na kizunguzungu pamoja na kuishiwa nguvu(uchovu)
 • Kupungua kwa msukumo wa damu
 • Kupauka pamoja na ngozi yake kuwa ya baridi

Namna ya kumpatia huduma ya kwanza mtu anayetokwa na damu:

 • Kwanza kabisa kama mgonjwa ana nguo basi zitoe nguo hizi ili sehemu ya jeraha au kidonda pawe wazi. Na pia kama utaweza kupata gloves ni vyema uzivae kabla ya kuanza huduma hii ili kujikinga na maambukizi yoyote yale.
 • Kama kidonda ama jeraha ni dogo, paoshe na maji safi alafu tumia vidole vyako kupagandamiza kidogo ukiwa na kipande cha nguo safi, gozi au pamba ili kupunguza damu kuvuja.
 • Kama kidonda ama jeraha ni kubwa mfano kwenye mikono au miguu, mlaze mgonjwa chini halafu nyanyua juu kidogo zaidi ya kichwa sehemu iliyoumia ili kupunguza kasi ya damu kutoka. Kisha weka kipande cha nguo safi, gozi au unaweza kutumia kiganja cha mkono wako kwa dakika kumi na tano ili kuzuia damu isiendele kutoka.
 •  Hii itasaidia damu kuganda kwa haraka zaidi. Kama mgonjwa yupo macho na anajitambua, mwambie ashike mwenyewe.
 • Na kama damu bado itaendelea kutoka, ongeza kiasi cha gozi au pamba na ufunge tena kwa bandeji  nyingine juu yake. Ila kuwa makini usipafunge sana maana inaweza kuzuia mzunguko mzuri wa damu sehemu hiyo.
 • Nia ya kutoa huduma hii ni kuzuia damu isiendelee kuvuja na kuisha mwilini.
 • Kisha muwahishe katika kituo cha afya au hospitali iliyo karibu kwa matibabu zaidi na dawa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center