Jua aina za allergy na jinsi zinavyosababishwa.

 

1. Allergy za dawa. Dalili za allergy hii ni kama ngozi kuwa na mabaka yanayowasha(hives), vipele na homa.

2. Allergy ya vyakula. Dalili za allergy za vyakula ni kama ngozi kuwa na mabaka yanayowasha(hives), matatizo ya tumbo kama kuharisha, kutapika , njia za hewa kuvimba(husababisha kuto kupumua kirahisi).

3.Allergy za kushika mahali au kitu(contact dermatitis).Ngozi huwa inawasha na huonekana nyekundu.

4. Latex allergy. Latex hutumika kutengeneza vifaa kama gloves, condoms. Hakikisha unakagua vifaa unavyotumia kama una allergy na latex. Dalili za allergy ya latex ni kama ngozi kuwasha na kubabuka na huweza kupelekea hali iitwayo shock(viungo vya mwili kukosa damu).

5.Allergy za wanyama, hasa manyoya ya wanyama kama paka, dalili ni kama kupiga chafya na kutokwa na makamasi.

6. Allergy ya mbegu za maua(pollen) na mold nyeusi. Dalili ni kama kukohoa, kutokwa na machozi, ngozi kubabuka.

7. Allergy za kung’atwa na nyuki, allergy za mafua n.k.

Ni vizuri kila mtu ajue ana allergy na kitu gani kwani allergy isipotibiwa ukiipata huleta hali mbaya zaidi iitwayo anaphylaxis. Hii huweza kupelekea shock(viungo vya mwili kukosa damu) ambayo huweza kupelekea kifo. Namna ya mtu kujua ana allergy na kitu ni kufanya allergy test hospitalini.

Privacy Preference Center