Muda sahihi wa kuanza usafi wa meno kwa mtoto.

Umewahi kujiuliza ni wakati gani hasa uanze kusafisha meno ya mtoto wako?!Na pengine ulishawahi kuogopa kutumia mswaki kwa mtoto hasa alie chini ya miezi 12. Na pengine umekua na tabia ya kutomsafisha meno mtoto, labda ni uoga au hofu ya kumuumiza lakini inaweza kuwa ni ngumu na mtoto kuwa msumbufu.

Huu apa ni muongozo juu ya usafishaji wa meno ya mtoto wako.

1.Muda sahihi kwa mtoto kuanza kusafishwa meno na kinywa ni pale tu jino la kwanza linapo ota, umri wa kuanzia miezi 6 mpaka miezi 8.

2.kuanzia Muda huo mtoto husafishwa meno na kinywa kwa kutumia kitambaa kisafi na laini chenye unyevunyevu, au mswaki laini wa watoto na maji peke yake usitumie dawa ya meno.

3.Zoezi hili huendelea chini ya usimamizi wa mzazi au mlezi mpaka umri wa mwaka mmoja na miezi sita.

4.Dawa ya meno huanza kutumika pamoja na mswaki mlaini kumsafishia mtoto meno kuanzia umri wa miaka miwili mpaka minne, Mara mbili kwa siku baada ya kuamka na kabla ya kulala usiku.

5.Dawa ya meno kwa mtoto wa kuanzia miaka 2 mpaka 4 ni kidogo tu kama punje ya haragwe, Usitumie dawa nyingi kwa mtoto.

6.Hakikisha unapomsafisha mtoto anatema ile dawa yote yaani asimeze dawa ya meno.

7.Na pia asisukutue na maji baada ya kumaliza kumswaki hii husaidia dawa kubaki juu ya meno na hulifanya jino kuwa imara.

10 thoughts on “Muda sahihi wa kuanza usafi wa meno kwa mtoto.

 1. Nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu hili suala, nashukuru leo nimejifunza.

  Ila nina swali moja
  Je hapo kwenye kutomsafisha na maji mtoto baada ya kupiga mswaki ili jino liwe imara, ni kwa watoto tu au hata sie wakubwa tunatakiwa tusisukutue na maji?

  1. Tunashauri hivyo hata kwa wakubwa, ukisha kupiga mswaki vizuri na kusugua ulimi wako basi ni vyema kutema tu povu la dawa lakini usitumie maji kusukutua ili dawa ibaki juu ya meno kwa muda kama nusu saa hii hulifanya jino kuwa imara zaidi kutokana na madini yaliyopo katika dawa.
   endelea kutufuatilia daktari mkononi.

 2. Nashukuru sana kwa elimu hii, nilikuwa muoga sana kusafisha meno ya mwanangu kwa kuhofia kumuumiza, Mungu awajalie zaidi @ daktari mkononi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center