Kifafa cha mimba (Eclampsia) ni nini?

Kifafa cha mimba kitaalamu hufahamika kama Eclampsia.Kifafa cha mimba (eclampsia) ni matokeo ya ugonjwa wa pre eclampsia.

Pre eclampsia ni nini?

Pre eclampsia ni pale ambapo mama mjamzito anakuwa na blood pressure ambayo ni kubwa kuliko kawaida(zaidi ya 140/90) na kuongezeka na protini kwenye mkojo.Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu na kuongezeka uzito,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction)

Eclampsia (kifafa cha mimba) ni nini?

pressure ikiendelea kupanda bila msaada wowote, mama pia hupata Seizures/convulsions(degedege/kifafa), na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).Sasa hizi dalili zikitokea (degedege/kifafa na kuchanganyikiwa) ndipo tunasema mama ana kifafa cha mimba.

Kifafa cha mimba hutokea wakati gani haswa?

Pre eclampsia na na kifafa cha mimba (eclampsia)hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.

Je kifafa cha mimba kinasababishwa na nini?

Chanzo cha huu ugonjwa bado haijulikani ni nini haswa,ila kuna baadhi ya mambo ambayo yatakayo kuweka hatarini kupata kifafa cha mimba navyo ni

  1. Kama ni mimba ya kwanza kwa mama
  2. Kama kuna historia ya eclampsia katika familia upande wako.
  3. Kama una chini ya miaka 20 au zaidi ya miaka 40 wakati wa ujauzito.
  4. Kama ulikuwa na tatizo la high blood pressure kabla ya ujauzito.
  5. Kama uzito wako ni mkubwa kulingana na urefu wako(overweight/obesity).
  6. Kama una historia ya eclampsia mimba iliyopita.
  7. Muda kati ya mimba. Kuwa na watoto chini ya miaka miwili au zaidi ya miaka 10 mbali husababisha hatari kubwa ya preeclampsia.
  8. Mimba ya mapacha au zaidi ya wawili.
  9.  Kama baba wa ujauzito huo ni mpya.

 

4 thoughts on “Kifafa cha mimba (Eclampsia) ni nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show