Mazoezi baada ya kujifungua

Wanawake wengi hupata mabadiliko ya kimaumbile na pia mwili huwa na mabadiliko ya homoni pale wanapojifungua. Kati ya mabadiliko hayo, wanawake wengi huhofia kuongezeka uzito kupita kawaida na kuwa na tumbo kubwa.

Mazoezi  husaidia kurudisha muonekano wa mama.Yapo mazoezi mengi yanayoweza kufanya hivyo.
Mazoezi baada ya kujifungua huwa na faida mbalimbali kama ifuatavyo;
-husaidia mwili kurudi hali yake ya mwanzo wa karibu na hali ile
-humsaidia mama kupata nguvu mapema
-husaidia kukaza misuli ya nyoga na tumbo
-humpa mama muonekano mzuri
-hupunguza mawazo ya uzazi na kukupa furaha.

Iwapo mama kajifungua hatakiwi kuwa na haraka ya kurudia hali yake ya mwanzo hasa kwa kufanya mazoezi mazito kwakuwa mwili wake umetoka katika hali ya tofauti na unahitaji muda kurudi, hivyo basi anaweza kuanza na mazoezi mepesi na kuongeza ugumu kadri anavyozidi kupata nguvu Zaidi.
Mazoezi haya huwa ya aina tatu ambazo ni:
1.Mazoezi ya tumbo hasa tumbo la chini, hapa utaanza na mazoezi mepesi yasiyoumiza misuli yako . mazoezi haya husaidia kuondoa mafuta yaliyojikusanya kipindi cha ujauzito. Mazoezi mengi hapa huhusisha pumzi . hapa mama huvuta na kutoa pumzi polepole huku akiwa kakaza tumbo. Mazoezi haya huwa magumu mwanzoni hivyo inashauriwa kuanza na nguvu kidogo na kuongeza kadri ya muda.
2. mazoezi ya nyonga; haya husaidia kukaza misuli ya nyonga na kuepusha matatizo kama kushindwa kubana mkojo .pia mazoezi haya husaidia kupona haraka sehemu ya nyonga na uke na kufanisisha mzunguko wa damu. Na hii hupunguza kuvimba baada ya mtu kuwa amejifungua kwa njia ya kawaida . mazoezi ya Kegel pia ni muhimu kwa mama baada ya kujifungua.
3. Kutembea ni zoezi la muhimu sana kwa mama aliyetoka kujifungua na inashauriwa kuwa mama aanze zoezi hili mapema Zaidi na inaweza ikawa hata masaa machache baada ya kujifungua. Hii inaepusha damu kuganda mpaka kumsababisha mama kutokwa damu. Kutembea kunamsaidia mama kupata nguvu mapema na kukaza misuli mingi zaidi. Inaweza kuwa anatembea kinyumenyume au zigzag kwakuwa itasaidia katika utendaji kazi mzuri wa misuli. Mama anaweza fanya hivyo iwapo tu anaendelea vizuri zaidi.
Ikiwa mama kapata nguvu ya kutosha na anendelea vizuri hivyo basi anaweza endelea na mazoezi ya nguvu zaidi kama push ups na kunyanyua uzito na mazoezi ya aerobic na anaerobic endapo anakuwa vizuri.

Muda gani unafaa kuanza mazoezi; kwa mama aliyejifungua kwa kawaida na hakupata shida yoyote wakati wa ujauzito na wa kujifungua anaweza anza mapema zaidi wiki ya 3-4 na kwa mama aliyejifungua kwa njia ya upasuaji hushauriwa kufanya mazoezi mepesi mpaka angalau baada ya wiki 6 ili kutoa muda wa kutosha kuruhusu mshono kupona kwa kuepusha shughuli nzito.
Vitu kama lishe nzuri husaidia katika uzito wa mama.
“Mama asiwe na haraka ya kupata mabadiliko maana inaweza mletea madhara badala ya faida bali afanye mazoezi pole pole kuruhusu mwili kubadilika wenyewe inavyostahili.

4 thoughts on “Mazoezi baada ya kujifungua

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show