Mazoezi yanayo saidia kupunguza maumivu ya kiuno

Baadhi ya Sababu za maumivu ya kiuno

1. Kukaa (kwenye kiti ,chini) kwa muda mrefu

2. Mkao mbaya mfano kukaa kwenye kiti bila kunyooka vizuri

3. Kazi ambazo zinahusisha kuinama kwa muda mrefu

4. Ajali au kuvunjika sehemu za chini za mgongo/kiuno

5. Magonjwa ya mifupa

Mbali na mazoezi yaliyo oneshwa kwenye video hapo juu njia zingine za kupunguza maumivu ya kiuno ni

1. Kutembeatembea. Unapopata maumivu ya kiuno usikae wala kulala , endelea kufanya shughuli zako ndogondogo za nyumbani. Hali ya kutembea inasaidia kupunguza maumivu.

2. Kujikanda na maji ya moto. Hii inasaidia mishipa ya damu kutanuka na kupeleka damu kwa wingi kwenye tishu. Inasaidia kupunguza maumivu.

3. Unaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu kama maumivu ni makali sana na kwa kupata ushauri kutoka kwa daktari.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center