Je, kuna tiba ya chunusi?

Wengi hujiuliza kama kuna tiba ya chunusi, kwa kumaanisha dawa au njia ambayo inaweza kutumika kumaliza chunusi kabisa. Kiukweli hamna tiba ambayo inaponya chunusi kabisa lakini kuna tiba zilizopo kwa ajili ya kupunguza athari na kupunguza makovu katika ngozi kutokana na chunusi. Malengo makubwa ya hizi tiba ni kumpunguza kujisikia vibaya kutokana na maumivu ya chunusi, kuboresha mwonekano wa ngozi, kuzuia makovu pamoja na kupunguza matatizo ya kisaikolijia kutokana na mtazamo wa jamii juu ya chunusi.
Matibabu ya chunusi yanajikita katika kuzuia chunusi mpya, chunusi na mabaka ambayo yalikuwepo kabla ya kuanza matibabu huisha taratibu ndani ya wiki au miezi kadhaa. Kulingana na wingi wa chunusi mabadiliko ya maana huanza kuonekana baada ya miezi miwili hadi miezi nane.
Vitu muhimu vya kuzingatia katika safari ya kutibu chunusi ni kama vifwatavyo:
1. Hupaswi kushika shika na kutumbua chunusi kwani hii huongeza uwezekano wa kuweka vijidudu mbali mbali usoni ambavyo vinaweza kuzidisha zaidi chunusi na kusababisha mabaka.
2. Ni muhimu kuosha uso mara mbili kwa siku kwa kutumia maji ya uvugu vugu na sabuni. Vile vile kutumia mild facial cleanser baada ya kuosha uso ili kuhakikisha ngozi ni safi kabisa. Kuosha uso mara kwa mara au kwa kutumia nguvu sana haishauriwi kwani inaweza kuleta madhara zaid kwa ngozi.
3. Inashauriwa kutumia mosturiser ambayo haina mafuta (oil free moisturiser) yenye kinga ya jua (spf 15 na kuendelea). Epuka vipodozi vyenye mafuta(Oil based).
Matibabu ya chunusi yaweza kuhusisha dawa za kupaka kama benzyl peroxide, tretinoin, isotretinoin au za kumeza kama antibiotics na homoni au zote za kupaka na kumeza kwa pamoja. Aina ya matibabu inategemea sababu na wingi wa chunusi. Ni muhimu kumuona daktari wa ngozi ili kuweza kupata matibabu yanayoendana na chunusi zako. Ni muhimu kufahamu kuwa chunusi haziponi, lakini matibabu yanapunguza au kudhibiti kabisa chunusi mpya hivyo mara nyingi muathiriwa atahitajika kujali ngozi yake siku hadi siku bila kuchoka hata baada ya kumaliza matibabu ili kuzidi kuwa na uso bila chunusi.

4 thoughts on “Je, kuna tiba ya chunusi?

 1. 😊😊asante sana hii swala
  La chunusi hata mm lilinisumbua mno na mba je kwenye nywele ?? Zinatokana na nn?? tiba yake pia kma ipo naomba ufafnuzi.

 2. Kuna vitu mbali mbali vinavyosababisha mba.
  1. Kuchangia vifaa vya nywele kama vitana na mtu ambae anamba wa nywele.
  2. Kutokuosha nywele na sabuni au shampoo mara kwa mara hujenga uchafu katika ngozi ya kichwa ambao husabisha mba
  3. Ukavu wa kupitiliza wa ngozi ya kichwa.
  4. Matumizi ya dawa ambazo zinashusha kinga ya mwili(mf. Predinisolone n.k)
  5. Nywele kuwa na unyevu unyevu muda mrefu kutokana na jasho au kuto kukauka vizuri baada ya kuoga.
  Mba za kichwa zinapona kabisa ukizingatia yafuatayo:
  1. Epuka kuchangia vifaa vya nywele na watu wengine.
  2. Osha nywele na shampoo ambayo inadawa ya mba kila siku asubuhi na jioni angalau kwa wiki mbili( mf. Ketoconazole shampoo). Kisha endeleza desturi ya kuosha nywele mara kwa mara na sababu au shampoo uipendayo.
  3. Endapo nywele ni ndefu sana inashauriwa kunyoa muda wa matibabu.
  4. Epuka ukavu wa ngozi ya kichwa kwa kupaka kiasi kidogo cha mafuta katika nywele baada ya kuosha.
  Endapo bado tatizo la mba litaendelea inashauriwa kumwona daktari kwa matibabu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show