Kupandikizwa kwa kondo la uzazi chini ya tumbo la uzazi (placenta previa)

Hii ni hali inayotokea pale kondo la uzazi linapo pandikizwa kwenye sehemu ya chini ya tumbo la uzazi.

Chanzo kikuu cha tatizo hili hakijulikani ingawa wanasayansi wanaamini kuwa huenda imesababishwa na mimba kupandikizwa sehemu ya chini ya tumbo la uzazi, kusambaa kwa tishu zinazoshikilia kijusi kichanga kuliko kawaida katika mji  wa mimba baada ya ukuta wa tumbo la uzazi kuwa na kasoro na kuwa na kondo kubwa la uzazi hasa pale mama anapokuwa na mimba zaidi ya moja.

Walio katika hatari ya kupata tatizo hili ni pamoja na:
1.mama aliyejifungua zaidi ya mara moja.
2.mama kuwa na umri zaidi ya miaka 35
3.historia ya kujifungua kwa upasuaji pamoja na kufanyiwa aina yoyote ya upasuaji katika tumbo la uzazi
4. uvutaji wa sigara
5. kusafishwa tumbo kwa njia ya curratage.

Dalili za ugonjwa:
1. kutokwa damu ukeni kuanzia wiki ya 28 ya ujauzito ambayo haiambatani na maumivu ya aina yoyote na haina chanzo chochote kinachojulikana. Damu hiyo huanza ghafla na mara nyingi hutokea nyakati za usiku na haimbatana na kufanya shughuli yoyote. Rangi ya damu huwa ni nyekundu mng’avu (bright red).

Madhara ya ugonjwa kwa mama:
1. upungufu wa damu kwa mama baada ya kutokwa na damu nyingi
2. kupata uchungu kabla ya mimba kufikisha umri wa kujifungua
3. mtoto kushindwa kujigeuza hivyo kukaa vibaya tumboni kulingana na umri wa mimba
4. kupasuka mapema kwa chupa ya uzazi
5. kondo la uzazi kubaki ndani baada ya kujifungua na kusababisha damu kuendelea kutoka bila kukoma
6. kuchelewa kufunguka kwa njia ya uzazi wakati wa uchungu
7. kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua

Madhara kwa mtoto:
1. mtoto kuzaliwa na uzito pungufu
2. mtoto kupata upungufu wa hewa ya oksijeni hali inayoweza kumletea mtindio wa ubongo.
3. mtoto kufia tumboni
4. kuumia kwa mtoto wakati anazaliwa kama kuteguka mikono na miguu

Matibabu:
1. mama anashauriwa kwenda hospitali mara moja aonapona dalili tajwa hapo juu kwani tatizo hili likiwahiwa mapema hutibika na madhara huwa kidogo kwa mama, mtoto na jamii kwa ujumla. Njia pendekezwa ya uzazi ni kujifungua kwa njia ya upasuaji kwani hupunguza madhara zaidi na huchukua muda mfupi hivyo kupunguza madhara ya ugonjwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center