Je, unasumbuliwa na ugonjwa wa UTI? Part1

Wanasayansi husema, “Mmoja kati ya wanawake wawili huwa na ugonjwa wa UTI.”

Kwa wanawake uwezekano wa kupata ugonjwa wa UTI ni mkubwa sana. Hii ni kwasababu ya jinsi maumbile ya wanawake yalivyo.

Nini huleta UTI?
UTI kwa ujumla hutokea pale bakteria ziingiapo katika mfumo wa mkojo

Dalili za UTI ni zipi?
Dalili za UTI ni kama zifuatavyo:-
•Kuumwa na tumbo la chini pamoja na maumivu ya nyonga.
•Kusikia kama haja ndogo inaunguza pale inapotoka.
•Kukojoa haja ndogo kwa kiasi kidogo mara kwa mara.
•Kukojoa mkojo ulio na ukungu.
•Kukojoa mkojo wenye rangi nyekundu au rangi kama ya cocacola.
•Kutoa mkojo wenye harufu kali.
•Homa

Nani yupo katika hatari ya kupata UTI?
•Wanawake kwa ajili ya maumbile yao.
•Wanawake ambao hujamiana mara kwa mara na ambao hubadilisha wenzi mara kwa mara
•Kuwa na upungufu wa kinga mwilini kama wagonjwa wa kisukari.
•Baadhi ya njia za kuzuia uzazi.
•Ujauzito.
•Uzee, hasa wanawake waliokoma hedhi.
•Pia kama umetumia dawa za antibiotiki siku chache kabla ya kupata UTI.

2 thoughts on “Je, unasumbuliwa na ugonjwa wa UTI? Part1

  1. Dokta, umesema inatokana na wadudu(bakteria) kuingia katika njia ya mkojo, na umesema pia kutumia dawa za kuua haohao wadudu (antibiotiki) inaweza kuwa chanzo cha tatizo. Na sielewi Zaidi kwa kuwa dawa hizohizo ndizo zinatumika kwa matibabu. Nisaidie.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center