Je, unasumbuliwa na ugonjwa wa UTI? Part2

Nini hutokea pale ambapo hutatibu UTI mapema?

•Ugonjwa kujirudia mara kwa mara.
•Figo kuharibika
•Kwa wanawake wajawazito, kujifungua watoto wenye uzito mdogo au kujifungua kabla ya miezi kutimia (njiti)

Kwahyo ni muhimu kutembelea kituo cha afya pale tu uonapo dalili zozote kati ya zilizotajwa

Nifanye nini kujiepusha na UTI?
•Kuwa na tabia ya kunywa vimiminika haswa maji mara kwa mara.
•Kumbuka kujifuta mbele kwenda nyuma mara baada ya kumaliza haja ndogo.
•Nenda chooni mara tu usikiapo haja ndogo na kila baada ya kujamiana.
•Epuka kutumia kitu chochote chenye kemikli maeneo ya ukeni.
•Epuka kutumia baadhi ya njia za kuzuia uzazi kama diaphragm.

2 thoughts on “Je, unasumbuliwa na ugonjwa wa UTI? Part2

  1. hivi kitu gani kinasababisha mwanamke kupata hedhi yake mara mbili kwa mwezi yaan mwamzo wa mwezi na mwisho wa’mwezi nndabya siku 28.

  2. Ahsante kwa swali, sababu zinazoweza kusababisha mwanamke kupata hedhi mara mbili kwa mwezi ni kama kutumia dawa za uzazi wa mpango, kuwa na mzunguko mfupi wa hedhi, na magonjwa mengine ambayo yanatokea kwenye viungo vya uzazi wa mwanamke kama fibroids. Ni vyema kumuona daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake mapema kwa uchunguzi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center