Kwanini mwanangu kafia tumboni ( sehemu A)

Moja kati ya taarifa ngumu kupokea kwa mama mjamzito na familia kwa ujumla ni ile ya kifo cha mtoto akiwa tumboni. Ni wakati wa majonzi uliojaa maswali mengi ya “nini kimetokea mwanangu akafa?”

Ziko sababu nyingi zinazoweza kupelekea mtoto kufia tumboni. Sababu hizi tunaweza kuzigawa katika makundi mbalimbali, na katika toleo hili tutaangalia namna ambavyo maambukizi ya magonjwa kadhaa yanavyoweza kusababisha vifo vya watoto tumboni.

Zifuatazo ni njia ambazo maambukizi yanaweza kuleta vifo vya watoto tumboni;

  • Mtoto akiwa tumboni hupata virutubisho anavyohitaji kwa ukuaji kutoka kwa mama kupitia placenta. Uchafu unaozalishwa kwenye mwili wa mtoto hutolewa kupitia placenta. Kuna baadhi ya maambukizi ambayo huishambulia placenta na kusababisha isifanye kazi yake kwa ufasaha hivyo kupelekea mtoto kukosa mahitaji yake muhimu kwa ukuaji Kama vile oksijeni na virutubisho vingine.
  • Mbali na njia hii; vijidudu vya magonjwa huweza kupita katika placenta na kusababisha maambukizi kwa mtoto pindi akiwa tumboni mwa mama yake bado. Kulingana hali kwamba ulinzi wa mwili wa mtoto haujakomaa ipasavyo, vijidudu hivi huvamia mifumo mbalimbali ya mwili wa mtoto na hata kuleta kifo.
  • Maambukizi ya magonjwa mbalimbali kwa mama mjamzito pia yanaweza kusababisha mama kuugua sana, mfano Homa kali na kupelekea mwili wake kushindwa kumpatia mtoto mahitaji yake Kama inavyotakiwa kwa ajili ya ukuaji.

Yapo magonjwa kadhaa yatokanayo na virusi, bakteria, na hata protozoa yanayoweza kuleta madhara tajwa hapo juu. Moja kati ya haya ni Malaria, ugonjwa ambazo wengi tunaupata mara kwa mara. Malaria kwa mama mjamzito ni hatarishi kwani vijidudu vya malaria vina uwezo wa kukua na kukusanyika kwenye placenta hivyo chakula na oksijeni kushindwa kufika kwa mtoto, pia mama huweza kuugua sana kupelekea kifo kwa mtoto. Magonjwa mengineyo ni Yale yaambukizwayo kwa njia ya ngono kama vile kaswende (syphillis) na kisonono( gonorrhea) n.k

Hivyo inashauriwa kwa mama mjamzito kuhudhuria kliniki mara kwa mara na kufuata maelekezo yote anayopewa na wataalamu wa afya. Kufika kituo cha afya mara aonapo dalili zozote au mabadiliko yoyote mwilini. Ni vyema pia kumjulisha mtoa huduma ya afya kama mtoto amepunguza kucheza. Ni jukumu la familia nzima kulinda afya ya mama mjamzito ili kupatamtoto kwa wakati na akiwa na afya bora.

Tukutane sehemu ya pili ya mada hii

2 thoughts on “Kwanini mwanangu kafia tumboni ( sehemu A)

  1. Rafiki yangu akiwa na ujauzito wa miezi 7 maji yalianza kumtoka mfululizo kwa siku kadhaa ukeni (chupa ilivunjika), alifanyiwa operation ili mtoto atolewe, mtoto alifariki masaa machache tu baada ya kutolewa,
    Swali….1-ni nini chanzo cha kutokwa na maji na hakuwa akihisi uchungu?
    2- ni nini chanzo cha kifo cha mtoto?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show