Uvutaji wa sigara: mkuki wenye makali kuwili

Kuvuta sigara ni sehemu ya buruduni na starehe kwa watu wengi. Ndani ya sigara kuna kemikali inayoitwa nicotine ambayo inasabisha mtumiaji ajisikie furaha, huongeza ashiki, hukuza utambuzi, hupunguza njaa, huongeza uwezo wa kujifunza, huongeza kumbu kumbu, hudhibiti hisia na hupunguza mawazo na mvutano.
Pamoja na yote hayo yanayofanya watu wavutiwe na sigara. Uvutaji wa sigara una athari nyingi katika afya ya binadamu.
1. Uvutaji wa sigara wa muda mrefu husababisha utegemezi kwa mtumiaji, mtumiaji anapokosa sigara kwa muda wa siku kadhaa anapata dalili za kuwa arosto kama hasira, wasiwasi, huzini, kukosa subira, ugumu wa kuzingatia na kukosa usingizi.
2. Moshi wa sigara unakemikali zinazo sababisha muingiliano wa kimetaboliki na dawa mbali mbali (mf. Insulin,propranolol), muingiliano huu hupunguza kiasi cha dawa kinachotakiwa kuwepo mwili. Hivyo ni muhimu kumjulisha mtoa huduma wa afya kama wewe ni mvutaji sigara ili kuepuka athari zozote na kuhakikisha tiba yako ni sahihi.
3. Matumizi ya tobako pia yanathari kadhaa katika afya ya mtu. Inaweza kusababisha magonjwa ya mapafu (mf. Empysema, kubanwa kwa pumu) , magonjwa ya moyo (mf. Shinikizo la damu), magonjwa ya uzazi (mf. Hupunguza uzazi kwa wanawake), magonjwa ya saratani (mf. Saratani za damu, kibofu, figo, mapafu n.k) na mengineyo.
4. Uvutaji wa sigara kwa wanawake wenye mimba pia huathari uumbaji na afya ya mtoto na huweza kusababisha mimba kutoka au kuharibika kabisa. Mtoto anaweza kuzaliwa na uzito mdogo kupitiliza na anaweza kufariki ghafla. Kutokana na hizi sababu mama mjamzito anashauriwa kuto vuta sigara kabisa.Ni muhimu kufahamu kuwa endapo wewe mwenyew sio mvutaji sigara. Kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa mtu mwingine anaevuta sigara pia inaathiri afya yako pia. Hivyo ni muhimu kwa mtu anaevuta sigara kusogea pembeni wakati anavuta sigara ili kuwalinda anaowapenda na jamii inayomzunga dhidi ya matatizo ya afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show