Damu katika mkojo huweza kusababishwa na saratani ya kibofu

Saratani ya kibofu cha mkojo ni saratani inayofuatia kwa kutokea mara nyingi kwenye jamii ya wanaume baada ya saratani ya tezi dume. Kibofu cha mkojo ni mfuko uliopo kwnye eneo la chini ya kiuno ambao umetengenezwa kwa misuli maalumu kwa kazi ya kupokea na kuhifadhi mkojo kwa muda kutoka kwenye figo, wakati wa mtu kujisaidia haja ndogo.

Je ni Sababu zipi zinazosababisha kupata Saratani ya kibofu cha mkojo?

1: KICHOCHO-kuugua kichocho utotoni ni moja ya sababu kubwa zinazoweza kupelekea kupata saratani hii.
2: KEMIKALI ZA VIWANDANI-baadhi ya watu wanaofanya kazi viwandani hasa vya kemikali, wapo katika Hatari pia. Viwanda vinavyotengeneza mipira, ngozi, nyaya na mafuta ya petroli vinahusika na saratani hii.
3:SIGARA-uvutaji wa sigara unachangia mara sita ya upatikanaji wa saratani hii ya kibofu cha mkojo.
4: SABABU ZA NJE-hivi ni kama mipira ya mikojo ya muda mrefu, kupata mawe katika kibofu cha mkojo pia huchangia
5: MAUMBILE-kuna baadhi ya watu walizaliwa kibofu cha mkojo kikiwa nje ya mwili, hii pia inachangia kupatikana kwa saratani ya kibofu

DALILI ZIPI HUASHIRIA SARATANI YA KIBOFU?

Saratani ya kibofu ni ni moja kati ya saratani zinazoweza kugundulika mapema kutokana na dalili zake pamoja na kuwahi katika huduma za afya, dalili hizo ni hizi zifuatazo..

1:Kutokwa na mkojo uliochanganyikana na damu, hii hali huambatana na kutokwa kwa vinyama vidogo vidogo pamoja na maumivu tumboni au chini ya kitovu. Mkojo uliochanganyikana na damu unaweza kutoka kila mara hadi kwa mwezi mmoja unapopata haja ndogo, ni muhimu kutafuta msaada zaidi wa kiafya uonapo ishara hii kwani inaleta upungufu mkubwa sana wa damu katika mwili(ANEMIA)
2:Kupata mkojo mara kwa mara ukiambatana na maumivu
3:Mkojo kuwa na harufu mbaya na kutoka kwa mawimbi
4:Kushindwa kuzuia mkojo pale unapokua unakojoa
5:Kuwa na mkondo wa mkojo dhaifu
6:Mkojo kukatika katika wakati unakojoa
7:Mara nyingine unakua na uvimbe chini ya kitovu
8:Kushindwa kumaliza kukojoa ilhali mkojo bado upo kwenye kibofu

Dalili hizi sio lazima mgonjwa awe nazo zote ila dalili hatarishi sana ni kupata damu au maumivu wakati wa kukojoa hivyo basi ni vyema kufuata msemo huu “UKIONA DAMU, MUONE DAKTARI”

Pia Saratani ya kibofu inaweza kukua na kusambaa sehemu nyingine za mwili hivyo kuwahi hospitali ndiyo inarahisisha tiba ya ugonjwa huu!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center