Fahamu kuhusu kisukari kinachosababiswa na mimba

Wakati wa ujauzito mama hupata matatizo mbalimbali ya kiafya, moja kati ya matatizo hayo ni pamoja na kisukari cha muda kitaalamu huitwa gestational diabetics. Hali hii hutokea wakati wa mimba tu na hupotea baada ya mama kujifungua. Hali hii husababishwa na ongezeko la sukari katika mzunguko wa damu kwa kipindi hiki cha ujauzito. Inakadiriwa zaidi ya 9.2% ya wanawake wajawazito hupata tatizo hili, hivyo ni muhimu kwa mama mjamzito kuhudhuria kliniki kwa ajili ya vipimo na ushauri zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya.

Mtu gani yupo katika hatari ya kupata kisukari cha ujauzito?
Kila mwanamke anaweza kupata tatizo hili, ila sababu zifuatazo zinamuongezea mama hatari ya kupata ugonjwa huu:
1. Mama mwenye zaidi ya miaka 25
2. Historia ya ugonjwa huu katika familia au mama mwenyewe kama ameshawahi kuupata kabla
3. Uzito na unene kupita kiasi

Je ni nini madhara ya tatizo hili la kisukari cha mimba?
1. Kupata mtoto mwenye uzito mkubwa, hivyo kupata shida wakati wa kujifungua na wakati mwingine hupelekea mtu kujifungua kwa upasuaji
2. Kujifungua kabla ya muda, kabla mapafu ya mtoto hayajakomaa hivyo husababisha mataizo ya upumuaji kwa mtoto.
3. Mtoto anaweza kupata tatizo la sukari ya kushuka baada ya kuzaliwa.
4. Tatizo la shinikizo la damu kwa mama na uwezekano wa kupata kifafa cha mimba.
5. Kisukari hiki chaweza kua cha kudumu endapo hakitatibiwa.

Je nifanye nini ili kuepuka kupata kisukari cha mimba na matatizo yake?
1. Hudhuria kliniki kwa muda uliopangiwa kwa ajili ya vipimo na ushauri.
2. Kula mlo kamili, tumia vyakula vyenye nyuzi nyuzi na epuka vyakula vyenye wanga na mafuta mengi
3. Fanya mazoezi walau dakika 30 kwa siku

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center