Goitre husababishwa na nini?

 

 • Upungufu wa madini joto (iodine) mwilini. Hii hutokea sana pale mtu anapokula mlo wenye Upungufu wa vyakula venye madini haya
 • Hutokea pia kipindi cha ujazito na mara nyingine kipindi cha ukuaji (kupevuka). Kwa sababu ya kuongezeka mahitaji ya madini joto haya.
 • Pia Kuna vyakula ambavyo husababisha goitre kama vikilwa sana/mara nyingi. Mfano cabbage.
 • Mara nyingine pia husababishwa na mwili wenyewe kutengeneza “chembechembe-askari ” ambazo hushambulia tezi na mwishoni kupelekea kuvimba (goitre)
 • Pia mara chache hisababishwa na uvimbe kwenye tezi. Uvimbe huo waweza kuwa ule usiosambaa au ule wa saratani.
 • Pia utumiaji wa chumvi isiyo na madini joto, inakufanya uwe katika hatari kubwa ya kupata goitre.

Karibu tuongee na tushauriane. Tuambie, je wewe wajua nini kuhusu goiter? ( katika sehemu hapo juu ya “comments”)

3 thoughts on “Goitre husababishwa na nini?

 1. Dokta,
  Kuna hii sababu ya matumizi ya vyombo vya plastiki, risiti za malipo vyenye kemikali ya bisphenyl-a na jinsi vinavyoweza kuathiri mifumo mbalimbali ya homoni. Homoni za uzazi na tezi ya thairoidi ndizo husemekana kuathirika zaidi na kuleta matatizo.
  Kitu kingine ambacho ni kama tetesi wanadai kemikali zinazofanana na homoni za uzazi katika vyakula, madawa ya kuua wadudu ni tatizo kwa homoni zetu.
  Ninyi madaktari mwasemaje?

  1. Ahsante kwa mchango wako.
   Kuhusiana na bisphenol- A, na utumiaji wa vyombo vya plastic hususani kwa tezi ya thairoidi, Kuna chunguzi mbalimbali ambazo zimefanyika hasa kwa wanyama kuhusiana na jambo Hilo. Na tafiti hizo zimeonyesha kunaweza kukakuwepo na uhusiano, kwa kemikali hizo kuzuia ufanyaji kazi wa hormoni ya thairoidi. Japokuwa, kwa upande wa binadamu bado hakuna tafiti madhubuti zinazoonyesha uhusiano huo. Bado ni tetesi kama ulivyosema. Lakini, bado tafiti zinafanyika katika suala hilo, na pengine hapa karibuni tutaweza kuona kwa uhakika kama jambo hilo ni kweli kwa binadamu kama ilivyo kwa wanyama wengine.
   Lakini, ushauri ni kwa wakati huu ni bora kujiepusha na kemikali hizo wakati bado chunguzi zinaendelea. Kwani “kinga ni bora kuliko tiba”.
   Ahsante

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center