Bawasiri (Hemoroidi) ilinitesa kwa kipindi kirefu (sehemu A)

Maumivu Yalivoanza – Maisha yangu yalibadilika, sikua na raha tena. Hakuna daktari alieanipa jibu zuri. Maumivu yalianza baada ya mtoto wangu kuzaliwa miaka 20 iliyopita. Niliongezeka kilo 25 nilipokuwa mjamzito. Maumivu niliyokuwa nikiyapata yalikua makubwa sana na yalikuwa yakija wakati nilikuwa natembea kwa muda mrefu au kwa umbali mrefu. Maumivu haya yalitokea katika njia yangu ya haja kubwa. Yalikua makali ila hayakukaa kwa muda mrefu, ndani ya dakika 5 yalipotea. Kwa sababu yalikua yakiondoka sikutiilia maanani sana tatizo hili. Siku moja niliamua kuwauliza mama na kaka yangu kama na wao hupata maumivu kama haya na wakasema ndiyo. Na hapo ndio ilikuwa mwisho wa mazungumzo nao. Nilijihisi vizuri kutambua kwamba sipo peke yangu.

Kuna siku nlienda hospitali na kumuuliza daktari ni sababu gani napata maumivu katika njia ya haja kubwa? Daktari akanianglaia kwa huruma, alijua hasa kile nilichokuwa nikisema. Alinielezea tatizo langu liliitwa bawasiri(hemoroidi) na aliniambia angeweza kunisaidia. Aliniambia kuwa alikuwa na wagonjwa wengi, wa kike na wa kiume ambao walipata dalili kama zangu.

“Ila ningependa kujua zaidi kuhusu bawasiri” nilimuuliza daktari wangu, na yeye bila kusita akaniambia kuwa bawasiri (au kama inavojulikana na wengi kama kuota nyama sehemu ya haja kubwa) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa haja kubwa. Bawasiri ni kati ya sababu kubwa ya kutokwa na damu katika haja kubwa. Tatizo hili sio hatarishi mara nyingi kwa afya na huisha lenyewe lakini mara nyingine huwa na maumivu makali na hukua na kutoka nje ya njia ya haja kubwa.

“Nini kilichosababisha bawasiri kwangu?” Niliendelea kumuuliza maswali na yeye akasema kuwa inawezekana nilipoongezeka uzito tatizo lilianza. Ingawa akasema kwa watu wengine sababu zingine ni kama Kufungika kwa choo (choo kuwa kigumu mara kwa mara) au kuhara, ukosefu wa mazoezi, visababishi vya lishe (chakula kilicho na kiwango cha chini cha faiba), ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio (asitisi, uvimbe ndani ya fumbatio, au ujauzito), jenetiki (kwa kurithi), kutokuwepo kwa vali katika vena ya hemoroidi, na kuongezeka kwa umri. Visababishi vingine vinayoaminiwa kuongeza hatari ni pamoja na unene, kuketi chini kwa muda mrefu, kikohozi kinachoendelea kwa muda na sakafu ya pelvisi kutofanya kazi.

Kichwani nilipata mawazo mengi, ila nilitaka kumuuliza daktari wangu kama tatizo hili linatibika. Siku poteza mda wowote na nikamuuliza

**itaendelea**

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center