Jinsi gani naweza kumsaidia mtoto wangu mwenye Kisukari

Watoto wengi huwa na aina ya kwanza ya kisukari lakini siku hizi kutokana na ongezeko la uzito mkubwa (obesity and overweight) kwa watoto, kumewafanya wanapata aina ya pili ya kisukari.

Mtoto anapogunduliwa na kisukari kwa mara ya kwanza; yeye pamoja na ndugu, jamaa na marafiki hupatwa na hali ya mshituko na hivyo huhitaji muda wa kuikubali hali hiyo na kufanya mabadiliko yatayofaa hali ya mtoto.

Hizi ni baadhi ya changamoto zinazoweza kutokea katika hatua zao za ukuaji

 • Mapokeo ya majibu ya kugunduliwa na kisukari

Mtoto agunduliwapo na kisukari kwa mara ya kwanza hupatwa na hisia mbalimbali kama mshtuko, hasira, kukataa, huzuni, woga au majuto. Hisia hizi hudumu kwa muda tu endapo mtoto atapata msaada unaostahili kutoka kwa marafiki, wanafamilia na wataalamu wa afya.

 • Kukabiliana na hali ya kuwa na kisukari

Kuishi na kusimamia kisukari kila siku ni jambo linalohitaji juhudi. Watoto huweza kupata hisia ya kuwa mzigo kwenye familia, kujiona wanapewa malezi tofauti na wenzao, kukabiliana na maswali ya wazazi wao kuhusu kula chakula na kuchoma sindano ya insulin na kuonewa wivu na ndugu zao wakidhani wanapendelewa. Mtoto akionesha kujisikia vibaya kutokana na haya ni vyema kupata msaada wa wataalamu.

 • Wakati wa shule

Wazazi wengi huwa na wasiwasi watoto wao wanapokua shule baada ya kugundulika na kisukari. Wakati wa shule ni muhimu kwa walimu kutambua kisukari pamoja na madhara yake, ni vizuri mzazi kutoa taarifa na mahitajiya muhimu kwa uongozi wa shule ili mtoto aweze kusaidiwa endapo atapata shida akiwa katika maeneo ya shule. Itapendeza zaidi mtoto akimtaarifu rafiki yake wa karibu hata mmoja kuhusu hali yake.

pendelea kumhusisha mtoto katika mchakato wote wa kukabiliana na hali yake ili kumjengea ujasiri na kujitegemea

2 thoughts on “Jinsi gani naweza kumsaidia mtoto wangu mwenye Kisukari

 1. Hivi kuna umri fulani ambao ndio mtoto anaweza kupata kisukari au anaweza kuzaliwa akiwa na kisukari?

  Ni vyema watoto wenzake na wanafunzi wenzie wakajulishwa juu ya mtoto mwenzao kuumwa kisukari?

  1. Mtoto aliye hatarini kupata kisukari huzaliwa na vinasaba hivyo mwilini lakini mara nyingi kuna zile triggers hasa za mazingira mfano kupewa maziwa ya ng’ombe katika umri mdogo, kuugua magonjwa ya virusi kama “mumps” ndo hupelekea kuanza kuoneshwa kwa dalili za ugonjwa.
   Mara nyingi huanza kuonekana mtoto akiwa na umri wa miaka 4 na kuendelea.

   Na kuhusu kuwajulisha watoto wenzie nimeeleza kwenye makala kwamba kuna umuhimu kwani inakua ni rahisi kumsaidia endapo atazidiwa kwani kutakua na mtu wa kuelezea kwanini hali hiyo imetokea
   Karibu tena

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show