jinsi ya kujichoma insulini mwenyewe.

Moja ya matibabu ya kisukari ni kutumia dawa ya insulini kwa njia ya sindano. Insulini inasaidia kufanya kiwango cha sukari kwenye damu kuwa kile kinachofaa mwilini.Hivo inashauriwa mgonjwa kujifunza namna ya kujichoma insulin mwenyewe na huwa maelekezo yanatolewa na wataalamu hospitalini au kliniki.

Maandalizi ya muhimu ni kama ifuatavyo;

  • Nawa mikono kwa maji safi na sabuni na jikaushe vizuri.
  • Andaa insulin na sindano yake(vuta dawa ya insulini kwa kuinamisha kichupa cha dawa kwa  kiwango kinachotakiwa ambayo ni 10u)
  • Safisha kwa pamba yenye sipiriti sehemu ambayo unajichoma sindano.
  • Shika ngozi yako kama inchi 1-2 ivi alafu choma sindano katika digrii 90(tazama kwenye picha pale juu)
  • Achilia ngozi baada ya kuchoma sindano kisha ichomoe sindano ,usisugue sehemu uliyojichoma Bali pakandamize kwa nguvu kwa kutumia gozi/pamba safi.
  • Tupa mahali sahihi sindano za pamba ulizotumia.

Kwa mtu anayechoma sindano ya insulin kila siku ni muhimu kubadilisha sehemu ya kuchoma sindano  (usichome sehemu moja kila Siku),kubadilisha eneo ni  muhimu kwasababu unapochoma eneo moja linaweza kupata uvimbe (lipodisytrophy )ambao unaweza kuzuia insulin kuchukuliwa vizuri na mwili hivyo kupelekea kiwango cha sukari kutokushuka hata baada ya kutumia insulin.

Sindano ya insulin inaweza kuchomwa maeneo kama:

  • Tumboni
  • Pajani
  • Mkononi na sehemu ya makalio.

Inashauriwa sana kuchoma sindano hii maeneo ya tumbo kwasababu ni sehemu rahisi kufikika na pia dawa inachukuliwa kwa uharaka zaidi na mwili. Unaweza ukawa unachoma Tumboni kila Siku  kwa kuacha inchi kadhaa na ulipochoma siku iliyopita .Epuka kuchoma maeneo yenye makovu ,kwasababu makovu yanaweza kuingilia mfumo wa insulini kuchukuliwa na mwili.

”Ishi kwa furaha na amani kwa kutumia dawa zako vizuri na kufuata ushauri unaopewa na wataalamu wa afya,kisukari inaweza kuwa historia ambayo si lazima iharibu kila sehemu ya maisha yako,chagua sasa njia sahihi ya maisha.”

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show