Kuna Haja ya Kupima Macho kwa Wagonjwa wa Kisukari

Athari za kisukari kwenye macho zinaweza sababisha kupungua kwa uwezo wa kuona na kutokuona kabisa.

Je ni wakati gani ukachunguzwe macho?

Kwa wagonjwa wenye kisukari cha aina ya pili/kisukari cha ukubwani (type 2 diabetes) wanatakiwa kupimwa macho pale tuh anapogundulika na kisukari.

Hii ni kutoka na madhara ya aina hii ya kisukari kutokea kwa kasi zaidi.

Kwa wale wenye kisukari aina ya kwanza/kisukari cha utotoni (type 1 diabetes) inashauriwa wapimwe macho ndani ya miaka 5.

Madhara ya kisukari kwenye macho huonyesha dalili pale uharibifu mkubwa ukishatokea

Hivyo ili kuokoa uwono wako,muone daktari wa macho mapema pale tuh unapogundulika na kisukari.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center