Rangi ni kielelezo muhimu cha hali ya Afya.

Rangi zimekuwa zikitumika katika maeneo tofauti tofauti kutoa maana mbalimbali. Mfano katika bendera ya taifa rangi ya kijani huonyesha uoto wa asili, njano humaanisha rasilimali zilizopo nchini kama madini, nyeusi huonyesha rangi adhimu ya wananchi na rangi ya bluu huonyesha vyanzo vya maji kama mito, maziwa na bahari. Hii ni sehemu tu ya matumizi ya rangi mbalimbali.

Katika maswala yahusuyo Afya kuna matumizi pia ya rangi mbalimbali katika utoaji wa huduma za Afya kama utoaji wa elimu ihusuyo Afya, vipimo, ushauri nk. Ni muhimu kwa kila mtu kutambua tofauti na maana za rangi mbalimbali katika maswala ya kiafya, hii itasaidi kumuwezesha mtu kuchukua hatua stahiki mapema iwezekanavyo endapo itaonekana rangi yoyote isiyo ya kawaida kwa mtu, hii inajumuisha rangi ya macho, ngozi, nywele, kucha nk.

Mwili wa binadamu ni muunganiko wa viungo mbalimbali kama ubongo, figo, ini nk, vyote hivi kwa pamoja hufanya kazi maalumu katika mwili na kukamilisha maana halisi ya maisha, miongoni mwa kazi za viungo hivi ni kusimamia usafirishaji wa taka mwili mpaka pale zinapotolewa nje ya mwili wa binadamu, miongoni mwa taka mwili hizo ni Haja ndogo(Maarufu kama Mkojo), mkojo ni kimiminika kitolewacho mwilini kikiwa na rangi zinazotofautina kati ya mtu mmoja na mwingine, utofauti huu unatokana na utofauti wa mfumo wa maisha kati ya watu. Kila rangi katika mkojo wa binadamu huonyesha maana fulani katika Afya ya mtu husika. Zifuatazo ni maana za rangi mbalimbali zihusuzo Afya katika haja ndogo.

•Haja ndogo isiyokuwa na rangi mithili ya maji safi. Haja ndogo ya aina hii inamaanisha kwamba muhusika ana kiwango kikubwa cha maji mwilini mwake, yaani anakunywa kiwango kikubwa cha maji kwa siku(au anatumia vyakula vyenye maji kwa kiasi kikubwa- chai, uji, supu nk), hali hii inaweza kupelekea uhitaji wa kujisaidia haja ndogo mara kwa mara(frequent urination) na kupoteza baadhi ya chembechembe muhimu katika mwili(body ions) kama Sodiam(Na)Potasiam(K) nk ambazo huchanganywa na maji na pengine ni maumivu ya kichwa. Hivyo kuna haja ya kupunguza kiwango cha maji uwapo katika hali hii, unashauriwa kutumia takribani maji lita mbili mpaka lita tano za maji kwa siku ili kuwa na Afya bora, lakini kwango hiki kinaweza kubadilika kulingana na hali ya hewa, kazi unayojihusisha nayo, aina za vyakula unavyokula pamoja na vinywaji.

•Haja ndogo yenye rangi ya unjano kwa mbali(Transparent yellow). Upatapo haja ndogo yenye rangi ya unjano kwa mbali inamaanisha kuwa mwili wako unakiwango sahihi cha maji, kiwango cha maji kinachotoka kinashabiiana na kiwango cha maji kinachoingia mwilini hivyo mwili upo katika hali nzuri ya Afya upande wa mahitaji ya maji, unashauriwa kuendeleza hali hiyo hiyo kwa manufaa ya afya yako.

•Haja ndogo yenye unjano mzito kidogo. Hali hii inaonyesha kuwa hali yako ya Afya ni nzuri, lakini unahitaji uongeze kiwango kidogo cha maji unayokunywa, hali hii ni kama utabiri unaoonyesha kuwa maji yazidi kupungua mwili hivyo kuna uhitaji wa kuyarudish kwa kuongeza kiwango kidogo cha maji unachokunywa.

•Haja ndogo yenye unjano mzito, rangi mithili ya Asali. Hapa unapaswa kunywa maji mengi kwa kua hali hii inamaanisha kuwa maji yaliyopo mwili hayakidhi mahitaji ya maji katika mwili yaani kuna kiwango kidogo cha maji, baadhi ya matokeo ya hali hii ni kichwa kuuma, kutoa mkojo wenye harufu kali na pengine matatizo ya figo. Hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kuongeza kiwango cha maji unachokunywa ili kuepuka haya matatizo.

•Haja ndogo yenye unjano mzito pamoja na weusi kwa mbali. Hali hii inamaana kwamba mwili upo kwenye uhitaji mkubwa wa maji kutokana na upungufu wa maji uliopitiliza(severe dehydration) pamoja na uwezekano wa kuwa na magonjwa katika ini, inashauriwa kuongeza kiwango cha maji unachotumia na endapo hali hii itaendelea basi onana na daktari kwa uchunguzi zaidi.

•Haja ndogo yenye rangi ya wekundu(Pink to reddish). Haja ndogo ya hali hii inapotokea ni vyema kuwa makini zaidi, pengine ni kutokana na aina za vyakula ulivyokula, mfano matunda aina ya bluberri(blueberries) huchangia rangi hiyo katika haja ndogo, lakini kwa upande mwingine inaweza kuwa kaishiria cha matatizo katika figo na mfumo wa mkojo kiasi cha kuruhusu damu kujichanganya na haja ndogo, onana na daktari uonapo hali hii.

Hizi ni rangi ambazo huweza kuonekana wakati wa kujisaidia, pia kuna rangi nyingine ambazo hazionekani sana katika haja ndogo kama kijani na bluu, lakini ni vyema ukatafuta ushauri wa daktari na vipimo zaidi endapo utagundua rangi isiyo ya kawaida pindi unapojisaidia haja ndogo, baadhi ya matatizo ya viungo kama figo, ini na mfumo wa mkojo yanaweza kuzuilika endapo yatagundulika mapema, Rangi ya haja ndogo inaweza kusaidia kwa njia moja au nyingine kutambua endapo unayo matatizo haya.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show