Tiba dhidi ya ugonjwa wa kisukari (Kisukari aina ya kwanza).


Kisukari ni hali ya mwili kuwa na kiwango kikubwa cha sukari(high blood glucose) kuliko kiwango kinachohitajika kwa matumizi mwilini, hali hii hutokea pindi mwili unapozalisha kwa kiwango cha chini au unaposhindwa kuzalisha kichocheo cha mwili(hormone) kitambulikacho kama Insulini, kichocheo hiki huwa kinasaidia mwili kutumia sukari yake kama inavyohitajika na kubakiza kiwango maalumu kinachozunguka katika damu.

Kisukari kipo katika aina mbili yaani kisukari aina ya kwanza na kisukari aina ya pili, matibabu ya kisukari yanategemeana na aina ya kisukari aliyonayo mgonjwa husika kwa kuwa kila aina ya kisukari inasababishwa na sababu zake maalumu.

Makala hii inaonyesha matibabu ya kisukari aina ya kwanza, MATIBABU HAYA YAFANYIKE CHINI YA USIMAMIZI NA MAELEKEZO YA MUHUDUMU WA AFYA.
Kwa aina ya kwanza ya kisukari kuna matibabu ya namna mbalimbali, matibabu yote huwa na lengo la kusaidia mwili kupunguza kiwango cha sukari mwili. Miongoni mwa matibabu hayo ni pamoja na;
β€’ Matumizi ya Insulini. Insulini hutumika kama dawa ya kisukari kwa wagonjwa wa kisukari aina ya kwanza kutokana na kiungo kinachohusika na kuzalisha insulini(kongosho- pancreas) kushindwa kufanya kazi yake, hivyo wagonjwa hawa huongezewa Insulini ili kusaidia mwili kuweza kusimamia na kupunguza kiwango cha sukari mwilini. Insulini haiongezwi mwilini kwa njia ya mdomo bali kwa kuchoma sindano maalumu za insulini(injection). Insulini utumika mara nyingi katika matibabu lakini kuna nyinginezo kama Sulfonylureas ambazo pia huweza kusaidia mwili kuzalisha insulini yake wenyewe.

β€’ Matumizi ya chakula bora. Wagonjwa wenye tatizo la kisukari wanapaswa kupata Chakula kilichoandaliwa chini ya usimamizi maalumu dhidi ya kiwango cha sukari, wagonjwa wa kisukari wanapaswa kuepuka matumizi ya vyakula aina ya wanga(carbohdrate) kwa kiasi kikubwa(vyakula hivi huongeza sukari kwa kiasi kikubwa mwilini) pamoja na vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda na juisi za viwandani( hata juisi zinazoandaliwa nyumbani zenye zenye sukari nyingi).

β€’ Mazoezi(kazi mbalimbali- physical activities). Mazoezi ni njia nzuri na muhimu katika kuimarisha Afya ya mtu dhidi ya magonjwa mbalimbali, vivyo hivyo hata kwa wagonjwa wa kisukari mazoezi ni sehemu ya matibabu, mtu anapofanya mazoezi huongeza uhitaji wa nguvu mwilini, nguvu hii huzalishwa pindi sukari iliyopo mwilini inapo vunjwavunjwa kwa kupitia mfumo maalumu mwilini wa kuzalisha nguvu(glucose metabolism), hivyo mgonjwa mwenye kisukari anapofanya mazoezi/kujihusisha na kazi mbalimbali huufanya mwili kuendelea kutumia kiwango cha sukari iliyopo mwili, hii husaidia kuzidi kupunguza sukari hii kidogo kidogo.
Ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa magonjwa ambayo hayatibiki, lakini ni ugonjwa unaoweza kutulizwa kabisa kiasi cha kudhani ya kwamba mgonjwa amepona, ndio maana wagonjwa wa kisukari hushauliwa kuchunguza kiwango cha sukari kila mara ili kuona kama kuna mabadiliko chanya katika tiba wanayoipta , upimaji huu wa kiwango cha sukari hutumia kifaa maalumu(glucometer). Ili kuweza kuutuliza ugonjwa huu mgonjwa na jamii inayomzunguka hawana budi kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na muhudumu wa Afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center