Hauhitaji nguvu nyingi kupiga mswaki 😊

Baadhi ya watu wanadhani kuwa kutumia nguvu nyingi wakati wa kupiga mswaki ndio njia sahihi ya kusafisha kinywa,lakini ukweli ni kwamba kusafisha kinywa kwa usadifu ni namna ambavo unasafisha na siyo mara ngapi wala nguvu unayotumia .Inashauriwa kutumia nguvu kiasi kidogo tu wakati wa kupiga mswaki.Je kuna madhara yeyote endapo utatumia nguvu nyingi?
Ndiyo, yapo madhara kama yafuatayo:

• Kupata vidonda na kuumia ; mara nyingi ukitumia nguvu nyingi ni rahisi kupoteza umiliki wa mswaki(control) na hivo kujigonga mdomoni na kwenye fizi,hii huleta maumivu ya kusababisha vidonda.
• Kuharibu muonekano wa meno yako: nguvu nyingi kupita kiasi inaweza Kuchubua sehemu ya nje ya jino(cervical abrasion) hii inaweza kupelekea sehemu ya ndani inayofuata(dentine) kuonekana , kwa kawaida ina rangi ya njano kuliko sehemu ya nje ya jino hivo kuonekana kwake kunaharibu mwonekano wa meno yako.

Kuchubuka kwa meno,fizi kulika

• Meno kupata ganzi na kuuma:endapo sehemu ya nje ya jino(enamel) imechubuka meno huwa yanapata ganzi au maumivu kila u apokula vyakula vya baridi au vya moto.
• Meno kuonekana marefu kuliko kawaida:hii inaweza kutokana na kuchubua sehemu ya juu ya fizi maeneo ambayo fizi inakutana a jino,fizi zikichubuka hushuka chini(gingival recession)
• Hatari ya kutoboka meno kirahisi:hii hutokea kama sehemu ya nje ikichubuka na hivo kufanya sehemu ya ndani kuonekana, kwa bahati mbaya sehemu hii ya ndani(dentine) siyo ngumu kama ile ya nje hivo huwa ni rahisi kutoboka.
Inawezekana kupiga mswaki ikawa ni mazoea tu lakini kuna baadhi ya vitu ni muhimu kuzingatia ili kuepuka matatizo mbalimbali ya kinywa na meno,unashauriwa kuzingatia yafuatayo unapopiga mswaki.
• Muda: tumia angalau dakika 2 mpaka 3 tu kupiga mswaki kuzidisha zaidi ya hapa kunaweza kusababisha mchubuko kwenye meno yako.
• Kutema dawa: unashauriwa usisukutue kwa maji ukimaliza kupiga mswaki badala yake tema dawa tu, hii husaidia dawa kukaa kwa muda kinywani na kuachilia madini ya floridi ambayo yanasaidia kutunza meno yetu,unaweza kunywa maji au kula baada ya angalau dakika 30 tangu ulipopiga mswaki.
Ushauri wa bure.

Unapotumia vimiminika vyenye asili ya asidi kwa mfano juisi ya ukwaju au malimao,ni vizuri kusukutua kwa maji baada ya kunywa ili kuiondoa ile asidi kinywani kwani asidi hii ikikaa muda mrefu kinywani inaweza kuchangia katika kuchubua meno yako.

Kwa taarifa sahihi na namna juu ya kupiga mswaki vizuri tafadhali pitia…http://daktarimkononi.com/2018/01/25/namna-sahihi-ya-kupiga-mswaki/

13 thoughts on “Hauhitaji nguvu nyingi kupiga mswaki 😊

 1. Nashukuru sana Doctor kwa ushauri na elimu nzuri unayotupatia kwa kweli inatusaidia sana hasa wale ambao hatuna uelewa juu ya jambo hili. Tutawaelimisha wenzetu kupitia Elimu hii ya bure.

 2. Thank you and God bless you all

  Naomba kujua pia njia nzuri katika kusafisha ulimi. Kwani nayo ni sehemu ya kinywa.

  Muda gani ninashauriwa zaidi kusafisha kinywa ?

  Kama kuna njia zingine za kusafisha kinywa (meno) tofauti na kitumia mswaki ?

  1. Asante August ni kweli ni muhimu kusafisha ulimi kama sehemu nyingine za mwili soma hapa kwa maelezo zaidi http://daktarimkononi.com/2018/03/05/safisha-ulimi-wako-epuka-harufu-mbaya-ya-kinywa/

   kuhusu kupiga mswaki ni kwamba mpaka sasa the gold standard of oral health is tooth brushing yani njia ya kuaminika,rahisi na inayoshauriwa kusafisha kinywa ni kupiga mswaki hivo tunashauri watu wapige mswaki kwa uweledi,pia muda mzuri wa kupiga mswaki ni asubuhi na usiku kabla ya kulala.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show