Kwa nini nimpe mwanangu dawa za minyoo?

Watoto wengi wapo katika hatari ya kupata minyoo. Katika michezo yao ya kila siku, wanakua wamekula vitu vingi vichafu kutoka kwenye udongo hasa hasa michezo ya makopo.  

Ni vigumu kuhakikisha mtoto hashiki uchafu huo, hivyo mtoto hula mayai ya minyoo ambayo husababisha ugonjwa wa minyoo. Minyoo hii ni kama Ascaris na Pin worms.  Minyoo hii inaweza ikampata mtu mzima kwa njia ya kuchangia vyoo hasa vya kukaa. Kwa hiyo mtoto anapopata dawa za minyoo itamkinga na minyoo na kupunguza maambukizi kati ya wanafamilia.

 

Dalili  za minyoo ni zipi?

1:Kikozi kisichotibika, mara nyingi minyoo huanza kwenda kwenye mapafu na kusababisha kikohozi kwa mtoto.

2: Mtoto kupungua uzito ghafla hata kama anakula vizuri.

3: Mtoto kujikuna kwenye matako mara kwa mara.

4:Mtoto anaweza akatapika minyoo endapo ugonjwa umekomaa sana. Na pia usiku minyoo wanaweza kutoka puani, msaidie mtoto kwa kumtoa huyo mnyoo polepole

5: Mtoto anaweza kupata maumivu makali ya tumbo kwa sababu ya minyoo iliyopo tumboni.

 

Hakikisha unamfikisha mtoto katika kituo cha afya unapoona mwanao anazidiwa. Usisahau kumpa mwanao dawa za minyoo.

1 thought on “Kwa nini nimpe mwanangu dawa za minyoo?

  1. Niliwahi kusikia kwamba minyoo inasaidia kutibu na kuzuia matatizo ya kuvimba kwa utumbo pamoja na utumbo wenye mwitikio uliopitiliza, inflamatory bowel disease na irritable bowels.
    Swali langu ni, je kutibu tibu minyoo kunaweza kupelekea matatizo haya?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show