Kuvimba kwa mfuko unaozunguka moyo (Pericarditis)

Moyo ni moja ya ogani muhimu sana mwilini na unazungukwa na mfuko ambao una kazi mbalimbali kama vile kuuweka vyema moyo katika sehemu yake,kuzuia moyo kutanuka ghafla kama damu imekuwa nyingi,kulainisha moyo na kuzuia maambukizi ya moja kwa moja kutoka kwenye ogani nyingine kama vile mapafu.

Kuvimba kwa mfuko huu huwa kunasababishwa na sababu mbalimbali zikiwemo zifuatazo

 • Maambukizi ya virusi,fangasi na bakteria
 • Kufeli kwa figo
 • Mshtuko wa moyo(Heart attack)
 • Kansa zinazosambaa kwa mfano kansa ya matiti na mapafu
 • Mionzi, kwa mfano ambayo anapata mtu wakati wa matibabu
 • Kuchomwa na kitu cha ncha kali kwenye kifua(eneo la moyo)
 • Kuna sababu nyingine pia tofauti na tajwa hapo juu kama vile dawa(procainamide,hydralazine,isoniazid,cyclophosphamide) na nyinginezo

Japo pia hutokea bila sababu zinazojulikana(Idiopathic)

Mgonjwa mwenye tatizo kama hili anakuwa na dalili zifuatazo

 • Maumivu ya kifua upande wa kushoto; Maumivu haya huwa yanasambaa kuelekea kwenye shingo,bega na mkono upande wa kushoto. Pia huwa yanaongezeka wakati wa kupumua.
 • Homa(Mwili kuchemka/Joto kuwa juu kuliko kawaida)
 • Kupumua kwa shida
 • Kukohoa na Kupata shida kumeza kama kisababishi ni kifua kikuu

Matibabu huwa yamejikita sana katika kisababishi, kwa hiyo uonapo dalili hizi na sababu hatarishi za mfuko wa moyo kuvimba ni vyema kuonana na wataalamu wa afya ili kujua tatizo na kupata huduma. Watu wengi huamua kutumia dawa bila ushauri wala usimamizi wa watalamu wa afya na kupelekea shida zaidi.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show