Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeathirika na sumu

Sumu ni hatari sana kwa binadamu, kwani ikiingia kwenye mwili huweza kusababisha uharibifu wa mwili na hata kupelekea kifo kwa mwathirika. Mtu anaweza kula sumu(mfano sumu ya panya) , kunywa sumu(mfano asidi au mafuta ya taa) au kuvuta hewa yenye sumu(mfano kuvuta hewa yenye moshi kwa mda mrefu). Endapo itatokea mtu amekula, kunywa au kuvuta hewa yenye sumu basi mwathirika huyu anaweza kuwa na dalili zifuatazo:

 • Maumivu ya tumbo
 • Kujiskia kichefuchefu na kutapika
 • Kuharisha
 • Kizunguzungu na kupoteza fahamu
 • Maumivu ya kichwa
 • Kupatwa na degedege
 • Kupumua kwa shida
 • Maumivu ya kifua
 • Kuchanganyikiwa kama kuona vitu ambavyo havipo au kusikia sauti ambazo hazipo.

Kama muathirika amekula au kunywa sumu na hajapoteza fahamu:

 • Haraka sana msafishe kinywa chake na maji mengi na hakikisha hakuna kitu cha hatari chochote kilichobaki.
 • Usimfanye mgonjwa atapike kwani kunaweza kuzidisha hatari, mfano mtu ambaye amemeza kemikali zenye uwezo wa kukwang’ua kama asidi.
 • Kama mgonjwa amepoteza fahamu, hakikisha kama bado anapumua kisha mlaze kiubavu.
 • Jitahidi kutambua ni sumu gani aliyotumia mgonjwa kama ni vidonge au vimiminika na kupeleka jina au sumu yenyewe kwa daktari, kisha umuwaishe mgonjwa katika kituo cha afya au hospitali iliyopo karibu.

Kama muathirika amevuta hewa yenye sumu:

 • Hakikisha kwanza mazingira ni salama kwako, kwani kama hewa ina sumu kali wewe mwenyewe unaweza kuathirika kama hauna vifaa vya kujikinga ipasavyo.
 • Kama ni salama,  kwa haraka mtoe mgonjwa na mweke nje kwenye mazingira yenye hewa safi au kama yupo ndani ya nyumba fungua madirisha na milango yote.
 • Toa nguo au kitu chochote ambacho mgonjwa amevaa karibu na shingo yake ili aweze kupumua vizuri na kwa urahisi zaidi.
 • Kisha mwahishe mgonjwa katika kituo cha afya au hospitali iliyokaribu na wewe kwa matibabu zaidi.

Kula au kunywa sumu ni njia amabayo mara nyingi hutumika katika kujidhuru au kujiua, lakini pia hutokea kwa bahati mbaya hasa kwa watoto bila ya wao kujua. Hivyo basi ni muhimu kuchukua hatua za awali ili kuzuia hatari hii kutotokea kwa kufanya yafuatayo:

 • Weka sumu na dawa zote mahali amabapo unajua watoto hawawezi kuzifikia kama kwenye makabati ya juu ukutani na kuyafunga kabisa.
 • Pia unaweza kuweka onyo kwenye sumu na dawa zote zilizopo katika mazingira yako, mfano nyumbani.
 • Usitumie vyombo vya chakula na vinywaji kwa ajili ya kuhifadhi sumu au dawa na pia usitumie vyombo maalum kwa ajili ya kuhifadhi sumu au dawa kwa ajili ya chakula au vinywaji

Kwa kufanya hivi basi wote kwa pamoja tutajenga mazingira salama zaidi kwetu sote.

3 thoughts on “Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeathirika na sumu

  1. Asante kwa swali lako zuri Fortunata, ni kweli kumpa muathirika maziwa fresh au hata maji ya kunywa husaidia. Lakini huduma hii inaweza kumpatia nafuu na kumsaidia muathirika yule tuh ambaye amekula au kunywa sumu, mfano mzuri asidi. Kwani ukimpa muathirika maziwa fresh haya yataenda na kudilute sumu ile na hivyo kupunguza makali ya sumu. Lakini pia hata baada ya kumpatia muathirika huduma hii bdo ni muhimu sana kumfikisha katika kituo cha afya au hospitali iliyopo karibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show