Mambo 6 muhimu ya kuzingatia kwa mtoto mwenye vipele vya joto.

Mambo 6 muhimu ya kuzingatia kama mtoto mwenye vipele vya Joto.

Vipele vya joto ni kati ya magonjwa ya ngozi ya kawaida kabisa ambayo hutokea kutokana na kuongezeka kwa joto, kama kumuweka au kutembea na mtoto sehemu zenye joto muda mrefu au mara kwa mara, kitaalamu huitwa heat rash.
Vipele vya joto huwa vyekundu na venye maji maji na hutokea hasa usoni, shingoni na sehemu ambazo muda mwingi zinafunikwa na nguo.
Husababisha mtoto kulia bila sababu hata kama amenyonya pia kushindwa kulala.

Hii hupelekea wasiwasi mwingi kwa mama na hupelekea kutaka kujua huduma ya haraka itakayo mpatia mwanae unafuu. Mara nyingi huwapata au hutokea kwa vichanga pamoja na wenye umri wa mwaka mmoja hadi minne.

Mambo 6 ya kufanya endapo mwanao ana vipele joto”

1.kumuosha eneo lenye vipele vya joto kwa maji na sabuni kisha kukausha kwa taulo safi.

2.kumvalisha nguo nyepesi za cotton epuka nguo za polyester na nylon.

3.kumuweka maeneo yenye upepo.

4.kutompaka cream or ointment sehemu zenye vipele.

5.kutokusugua sehemu zenye vipele vya joto.

6.hakikisha mwanao anakunywa maji ya kutosha au kumnyonyesha kila anapohitaji.

Je ni muda gani nimpeleke mwanangu hospitali?”

-Kama vimedumu kwa siku 3 hadi 4.

-Kama vinasababisha mtoto kujikuna sana.

-Kama vimeanza kuvimba na kujaa usaa.

-Kama ameanza kupata homa.

-Kama ameanza kutapika.

ย Ukiweza zingatia mambo hayo 6 muhimu na vipele vya joto vikapona venyewe na pia muwahishe mwanao haraka hospitali au katika kituo cha afya kilichopo karibu kama ana dalili zilizotajwa juu.”

 

Privacy Preference Center