Masharti muhimu baada ya kung’oa jino

Je, nisukutue na maji ya chumvi ili kuzuia damu isiendelee kutoka? Je ni lazima kutumia dawa ya maumivu baada ya kung’olewa jino? Baada ya kung’olewa jino utapewa maelekezo ya kufuata. Daktari pia anaweza kukupatia dawa ya maumivu kama kuna umuhimu wa kufanya hivyo. Ni vyema kusikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na daktari baada ya kung’oa jino. Hii itakusaidia kuzuia matatizo yanayoweza kutokea baadaye. Baada ya kung’olewa jino zingatia yafuatayo;

   Ng’ata  pamba uliyowekewa na daktari kwenye pengo kwa mda usiopungua nusu saa,baada ya hapo unaruhusiwa kuitoa mdomoni. Hii husaidia kuzuia damu kutoka na kuwezesha damu kuganda.Baada ya kutoa pamba damu itaendelea kutoka kdogokidogo  hata kwa masaa kadhaa.

Usipitishe kidole wala ulimi katika pengo maana unaweza kupelekea kuondoa damu iliyoganda (blood clot) ambayo husaidia pengo kupona haraka.Kupeleka kidole au ulimi  huweza  kusababisha  maambukizi katika pengo (infected socket).

  • Usile vitu vya moto wala vya baridi sana,hakikisha chakula ni laini na cha uvuguvugu (hasa siku ya kwanza baada ya kung’oa jino).Vyakula vya moto huweza kusababisha wewe kujiunguza sehemu yenye ganzi pia huweza kusababisha kuanza kutoka damu katika sehemu ya kidonda.
  • Usipige mswaki mara tu baada ya kungo’olewa jino ,na kesho yake usipitishe mswaki ndani ya pengo.Mswaki unaweza kutonesha kidonda na kusababisha damu kuvuja na maumivu.

 

Usipitishe kidole wala ulimi katika pengo maana unaweza kupelekea kuondoa damu iliyoganda au hata kusababisha kupeleka maambukizi katika  kidonda.

ENDAPO utapata tatizo lolote baada ya kung’oa jino kama maumivu makali,damu isiyoisha au shida nyingine yoyote hakikisha unamuona daktari kwa ushauri na/au matibabu zaidi.

8 thoughts on “Masharti muhimu baada ya kung’oa jino

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center