Imarisha mahusiano yako kwa mazoezi.

Mahusiano ni jambo muhimu sana katika maisha ya binadamu. Mazoezi huwaleta watu pamoja na kuongeza uimara wa mahusiano yao. Kibaiolojia mazoezi yana mchango mkubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi.

Zifuatazo ni namna ambazo mazoezi huimarisha mahusiano ya kimapenzi.

1. Kuongeza stamina katika tendo la ndoa.
Mazoezi huboresha mzunguko wa damu katika mwili, hivyo kupelekea usambazwaji mzuri wa damu na virutubisho muhimu mwilini.Mzunguko mzuri wa damu ni muhimu sana katika tendo la ndoa na afya kwa ujumla.

2. Mazoezi huongeza ashiki ya mapenzi.
Mazoezi ni moja ya visabishi muhimu katika utolewaji wa homoni za kike na kiume(estrogeni na testosteroni). Homoni hizi ni vichochezi vikubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa.

3. Mazoezi hutengeneza muonekano (maumbile) mzuri wa mwili. Hii huongeza mvuto kwa mwenza na hali ya kujiamini.

4. Mazoezi(kegel) hukaza misuli ya uke. Hii hupelekea kufurahia zaidi tendo la ndoa. Kujua jinsi ya kufanya mazoezi haya( kegel) tafadhari pitia posti ya nyuma katika kipengele hiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show